NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ndogo ya soka ya KMKM imeondoka na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Mchangani Kids inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya Kati, Unguja.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Mchangani majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa waushindani ambapo hadi timu hzo zinakwenda mapumziko hakuna timu iliofanikiwa kuzivaa vyavu za mpinzani wake.

Kurudi uwanjani kumaliza kipindi cha pili timu hizo zilifanya mabadiliko kurekebisha kikosi chake mabadiliko ambayo yalipeleka mafanikio kwa timu ya KMKM baada ya Ibrahim Machano kuifungia timu yake mnamo dakika ya 57 huku bao la pili likifungwa na Omar Thani katika dakika ya 78.