ZASPOTI
KOCHA wa Rwanda, Vincent Mashami, amebainisha changamoto ya timu yake kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Cameroun 2020 ambayo itaanza Januari 16 hadi Februari 7, 2021.
Mashami, aliyasema hayo baada ya kutangazwa kikosi cha wachezaji 31 ambacho kitaanza maandalizi ya michuano hiyo.


“Kipaumbele changu cha juu ni kuisaidia Amavubi kufika robo fainali. Nimewaambia wachezaji kwamba lazima tuvutie na kufanya hivyo itatuhitaji kufuzu hatua za mwisho za michuano hiyo”, alisema, Mashami.
Wachezaji wa Amavubi wameingia kambini baada ya kupimwa virusi vya ‘corona’.


Kati ya wachezaji 31, kumi na moja wametoka APR FC, wanne wanatoka Rayon Sports, watano wameitwa kutokea AS Kigali, Police FC ina sita, Kiyovu ina watatu wakati Musanze FC na Gasogi United wana mmoja.
Amavubi ipo katika kundi ‘C’ na Morocco, Uganda na Togo.
Kikosi hicho kitaanza kampeni yao ya makundi dhidi ya Uganda kabla ya mabingwa Morocco na watamaliza mechi zao dhidi Togo.


“Ni kundi gumu, lakini pia nadhani tuna uwezo wa kupita katika hatua ya makundi. Na, hiyo itakuwa lengo letu kuu”, alibainisha.
Wakati huo huo, Mashami, ambaye alikuwa kocha msaidizi wakati wa michuano ya CHAN 2016, atakuwa akikabiliana na bosi wake wa zamani, Johnny McKinstry ambaye sasa anaifundisha Cranes za Uganda.
Rwanda ilifanikiwa kuingia kwenye matoleo matatu mfululizo ya mashindano ya bara la Afrika.


Tangu kuanzishwa kwa CHAN mnamo 2009, Rwanda imekosa tu toleo la uzinduzi na mashindano ya 2014, ikifanyika kwa mara ya kwanza mnamo 2011 kabla ya kuandaa onyesho la 2016 na kufuzu kwa toleo la sita.
Lakini, utendaji mzuri wa nchi kwenye mashindano hayo ni robo fainali mwaka 2016. Amavubi aliindolewa kutoka hatua ya makundi kwenye matoleo ya 2011 na 2018.


Kikosi cha awali cha wachezaji 31 ni Yves Kimenyi (SC Kiyovu Sports), Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye (AS Kigali), Olivier Kwizera (Rayon Sports) na Umar Rwabugiri (APR FC).
Walinzi ni Thierry Manzi (APR FC), Ange Mutsinzi (APR FC), Hervé Rugwiro (Rayon Sports), Aimable Nsabimana (Police FC) na Fitina Omborenga (APR FC).
Wengine ni Emmanuel Imanishimwe (APR FC), Eric Rutanga (Police FC), Faustin Usengimana (Police FC), Emery Bayisenge (AS Kigali), Michel Rusheshangoga (AS Kigali) na Ally Serumogo (SC Kiyovu).


Viungo ni Olivier ‘Seif’ Niyonzima (APR FC), Eric Ngendahimana (SC Kiyovu), Martin Fabrice Twizeyimana (Police FC), Eric Nsabimana (AS Kigali), Djabel Manishimwe (APR FC), Dominique Savio Nshuti (Police FC) na Rachid Kalisa (AS Kigali).


Washambuliaji ni Lague Byiringiro (APR FC), Ernest Sugira (Rayon Sports), Danny Usengimana (APR FC), Jean Bertrand Iradukunda (Gasogi United), Osée Iyabivuze (Police FC), Justin Mico (Police FC), Jacques Tuyisenge (APR FC), Muhadjiri Hakizimana (AS Kigali) and Onesme Twizerimana (Musanze).
Makundi ya michuano hiyo ni Cameroun, Zimbabwe, Burkina Faso na Mali (kundi ‘A’),


Libya, DR Congo, Congo na Niger (kundi ‘B’), Morocco, Rwanda, Uganda na Togo (kundi ‘C’) na Zambia, Guinea, Namibia na Tanzania.(kundi ‘D’). (New Times).