Imeandaliwa na Sheikh; Yasser Mohammed Fahmy

Mjumbe wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri

Dar es Salaam, Tanzania

SHUKRANI zote anastahiki kuabudiwa yeye Mwenyezi Mungu bwana wa ulimwengu wote na Mtume Muhammad (SAW) ni mjumbe wake.

Mwenyezi Mungu Amehimiza sana kujitolea kwa ajili ya nchi ambapo kuipenda nchi ni sifa mojawapo sifa za kimaumbile wanayo wanadamu wote, kwa hiyo Mtume wetu alishtuka aliposikia kutoka Waraqa bin Noufal kwamba watu wake watamalazimisha ahamie nchi yake kwa kuwa anaipenda sana na amekuwa hataki kuihamia kabisa, na alipokuwa akitoka alisema kauli yake: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Makka ndiko nchi bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kwangu pia na angalau watu wake wamenilazimisha nihamie nisingetoka hata kidogo

Na kuipenda nchi si sifa ya wanadamu tu, bali wanyama pia, kwa hiyo si jambo la kushangaza kuwa sheria imekuja kuwahimiza wananchi kuipenda na kuitetea na kupigana kwa ajili yake hata mmoja akipotezwa na maisha yake huwa na fadhila kubwa nayo ni kuwa shahidi aliyekufa kwa ajili ya nchi yake, ambapo shahidi huyu amepewa cheo cha juu kabisa na kutunukiwa na Mwenyezi Mungu na watu pia, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia yaMwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakininyinyi hamtambui} [2/154].

Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu Amewaruhusia wananchi kutangaza upendo wao kwa nchi na kuwa wako tayari kufanya lolot kwa ajili ya nchi hiyo, hata ikiwa ni kupigana na wale wanaotaka kaiharibu nchi na kuwatokeza watu wake kutoka makwao: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu,na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu} [60/9].

Wakati huo huo Mwenyezi Mungu Amewaelekeza waumini kuwapenda na kuamiliana na wale wasiofanya uadui wowote dhidi ya nchi kwa wema na uadilifu hata wakiwa si waislamu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema nauadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [60/8].

Kwa hiyo tunaona kuwa uzalendo na kuipenda nchi katika sheria ndiyo sababu ya kupenda ama kutopenda na chanzo cha kujitolea na kujitahidi kuzuia madhara yoyote dhidi yake nchi tunakotoka. Inafahamika kuwa matini nyingi katika Qurani na Sunna za Mtume zimesisitiza ukweli wa kwamba uzalendo na kuipenda nchi ni sehemu ya imani inayotokana na maumbile ya kibinadamu, na kwamba hisia za upendo kwa nchi ni sifa inayopatikana kwa kila mwenye mwenendo ulio sawa na akili timamu, hata akiwa anaishi nje ya nchi yake hiyo.

Maumbile haya ya kuipenda nchi na kuwa na hamu kuinusuru na kuitukuza ni yale yale kwa wanadamu wote kwa dini mbalimbali, uraia tofauti, makabila mbalimbali n.k. Kwa hiyo Uislamu ulitambua haki ya kuipenda na kuitetea nchi kwa waislamu na wasio waisalamu, ambapo wote wanawajibika kuinusuru nchi na kusaidiana pamoja kulinda nchi yao bega kwa bega. Pia, heshima ya nchi ni sehemu ya heshima ya mtu kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alisisitiza kuwa: “Ye yote anayeuliwa akiwa anatetea heshima yake au mali zake au jamaa zake au ardhi yake basi huyu ndiye shahidi” Inafahamika kuwa ardhi ndiyo nchi.

Kwa hiyo tunatakiwa kuachana na hitilafu na migongano ya mitazamo na maoni na badala ya hayo tushirikiane na tufanye pamoja kuinua nchi katika nyanja mbalimbali na kushikamana kwa lenga la kuendeza nchi na kuyatatua matatizo yake.

Wala hatusahau mchango wa mwanamke na nafasi yake kufanikisha juhudi za maendeleo na ustawi wa nchi, ambapo mwanamke ndiye nusu ya jamii ambaye anawalea nusu wengine na kuwafundisha kuanzia uchanga mpaka uzima.

Kwa hivyo mwanamke ana mchango ambao hausahauliki kujenga ustaarabu na kuimarisha hali ya jamii na nchi.

Uzalendo mzuri wa kweli unatokana na Uislamu ambapo mafunzo ya dini hiyo na malezi yake ambapo mmwislamu hulelewa tangu utotoni awe anaipenda nchi yake na kuwa mwananchi mwema kwa nchi yake kwa kuzingatia pande zote za uzalendo ambazo zinajumuisha miamala mazuri pamoja na wananchi wote ambao ni waislamu na wasio waislamu na kutunza haki na wajibu na kulazimikia misingi ya jamii na maadili yake pamoja na kuheshimu mifumo ya utawala wake.

Pia, uzalendo unajumuisha vitendo vyote vya kuisaidia nchi ifanikiwe katika mikakati ya maendeleo yake na kuzihifadhi maliasili zake na vyanzo vya utajiri wake.

Jambo ambalo linawasaidia wananchi wapate manufaa makubwa kwa umma wote kwa sababu ya kuiweka nchi mbele. Miongoni mwa misingi ya uzalendo bora kwa mtazamo wa Uislamu kuamiliana na watu wote kwa usawa na undugu bila ya kujali tofauti zilizopo baina ya mtu na mwingine kama vile dini, rangi, kabila, itikadi, elimu, falsafa n.k. kwa kuwa jamii hujengeka tofauti huu ndo maana watu wakijibana katika makundi makundi waislamu wawe pamoja wakristo wawe pamoja au waafrika wawe pamoja na wengine wawe pamioa pasipo ushirikiano wowote au mshikamano wowote basi ufisadi mkubwa huwa katika jamii.

Kwa hakika uzalendo ndiyo maendeleo maana wananchi wote wanatakiwa kuwa na umoja na wajitahidi pamoja kuimarisha nchi na kuendeleza jamii. Katika Uislamu wananchi wote wana wajibu na haki sawa sawa, wote wanatakiwa kushirikiana kulinda nchi kutoka kwa maadui, wote wanatakiwa wazalisha na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao, wote wanatakiwa kuwa na uhusiano mzuri ambao unategemea ushirikiano na kukamilishana kwa kuwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Alipowaumba watu aliwaumba tofauti tofauti kwa hekima maalumu ambayo ni kukamilishana na kusaidiana kuimarisha ardhi na kuendeleza maisha.

Siyo sahihi kwamba Uislamu hauwaruhusia wafuasi wake kuamiliana na wafuasi wa dini nyingine au kwamba mwislamu anatakiwa kutengana na watu, bali kushirikiana ndiko msingi muhimu miongoni mwa misingi ya jamii ya kiislamu.

Pia, historia inatwambia na kutupa sura nyingine ya kuelezea hali ya Uislamu kushirikiana na wengine katika nyanja mbalimbali hasa biashara mpaka wakati wa vita, hali ilivyokuwa baina ya waislamu na wasio waislamu kutoka Ulaya na pengineko ambapo mikataba na biashara zilifanywa baina ya pande mbili japokuwa vita.

Uislamu ulisisitiza katika matini nyingi za Qurani na Sunna kuwa hekima ya kuumbwa kwa wanadamu katika jinsia, mataifa na makabila tofauti tofauti ni kujuana na kutambulikana ili wakamilishana na kubadilishana mawazo, uzoefu na manufaa na kwamba msingi wa kupendeleana baina ya watu ni uchamungu tu. Mwenyezi Mungu (S.W.) alisema: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana namwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari} [49/13].

Kwa hiyo, tunaona kuwa sheria ya kiislamu imetangaza kuwa watu wote wako sawa ambapo wametoka chanzo kimoja wakaumbwa na Mungu Mmoja watarejea kwake ili wafanyiwa hesabu kwa mema na maovu. Pia, sheria inawakumbusha waislamu kuwa wanatakiwa kuwa na uhusiano mzuri na watu wote na wasiwadharau wengine, bali washirikiane na watu wote kwa ajili ya kuhakikisha matarajio yao na kupata radhi ya Mola wao Mtukufu.

Kwa jumla uzalendo ni msingi mojawapo misingi ya maendeleo kwa kuwa tukiangalia jamii zilizofanikiwa kufika maendeleo tutambua kuwa wananchi wake wote wanasaidiana na kushikamana kuhifadhi uzalendo baina yao na kukamilishana katika juhudi za kujenga nchi yao na kuboresha hali ya maisha yao.