NA MWAJUMA JUMA

KOCHA wa timu ya soka ya wanawake ya Ladies Fighter Khadija Omar Suleiman amesema, kipigo walichokipata kimetokana na wachezaji kuwa majeruhi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati yake na Feature Queens ambapo alifungwa bao 1-0, ikiwa ni mchezo wa michuano ya kombe la Mapinduzi uliochezwa Mao Zedong.

Alisema  pamoja na kufungwa lakini amekubaliana na matokea hayo na kujipanga kwa ajili ya michezo ilinayofuata.

“Kiukweli nimefungwa nimekubali lakini ndio mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji wamejitahidi, lakini huu ni mchezo na kama ni mchezo nakubali matokea”, alisema.

Nae kocha wa timu ya Feature Queens Bizume Kassim amesema amefurahia ushindi huo na wachezaji wake wamefanya vizuri huku akivutiwa na jinsi walivyokuwa wakipokea maelekezo yake.

Alisema  wachezaji wake wamecheza vizuri na walikuwa wakifuata vyema maelekezo yake.

Michuano ya kombe la mapinduzi kwa soka la wanawake ni mara ya kwanza kufanyika, ambapo jumla ya timu tisa zinashiriki.