NA ZAINAB ATUPAE

DAKTARI wa timu ya soka ya KMKM Mwalim Haji Omar, amesema wachezaji waliokuwa wakisumbuliwa na majeraha katika timu hiyo wameanza kupata nafuu na kuungana na wenzao kuendelea na majukumu yao.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko Maisara, alikuwa na majeruhi wengine lakini ambao walikuwa wakisumbuliwa ni watatu.

Akiwataja majeruhi hao amboa walikuwa na matatizo yaliyopelekea kukosa mechi zote ambazo walicheza msimu huu ni pamoja na Mshambuliaji Mussa Ali Mbarouk.

Alisema alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyama ya paja ambalo lilimsababishia kukaa nje kwa miezi mitatu.

Alisema mchezaji mwengine ni Ali Juma Maarifa, ambae alikaa nje kwa muda wa wiki mbili alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kiwiko cha mguu, Suleiman Mohamed, ambae anasumbuliwa na tatizo la mguu na Salim Mussa Baja ambae alikuwa kaisumbuliwa na goti.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mshambuliaji Mussa Ali Mbaroku, alisema sababu ya kupoteza mchezo wa kwanza ni kukabiliwa na majeruhi wengi lakini anaamini kwa sasa watafanya vyema na kuongoza ligi hiyo.