LONDON,UINGEREZA

UMOJA wa Ulaya, EU na Uingereza zimekubaliana juu ya nyongeza ya kipindi cha miaka sita kabla ya kuweka ushuru kamili wa forodha kwa magari ya umeme na yanayotumia nishati na mafuta yaliyotengenezwa kwa vipuri kutoka nje ya maeneo hayo mawili.

Katika makubaliano ya biashara huria yaliyofikiwa,kimsingi hakutakuwa na ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazouzwa kati ya Uingereza na EU kuanzia Januari mosi.

Hata hivyo, vipuri vya kutosha kutoka nchini humo vinahitajika ili kufikia kigezo cha kutotozwa ushuru huo.

Kwa magari,ushuru huo unawekwa ikiwa uwiano wa vipuri kutoka nje ya eneo hilo vilivyotumika katika magari yaliyomalizika kutengenezwa unazidi asilimia 45.

Uingereza na EU zilikubaliana juu ya mpango wa awamu wa miaka sita kwa magari hayo.

Makampuni ya kutengeneza magari ya Japani kama Toyota Motor na Nissan Motor hutengeneza magari ya umeme na yanayotumia nishati na mafuta kwa kutumia vipuri vinavyoagizwa kutoka Japani.

Makampuni hayo yatahitaji kuongeza vipuri vyao ili kuepuka ushuru wa forodha utakaotozwa baadaye.