LILONGWE, MALAWI

Waziri wa Afya wa Malawi Khumbize Kandodo Chiponda

SERIKALI ya Malawi imetangaza kufunga mipaka mara moja kwa siku 14 wakati nchi hiyo ikishuhudia ongezeko la kasi la kesi za maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri wa Afya wa Malawi Khumbize Kandodo Chiponda alitangaza hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika mji mkuu, Lilongwe.

Pia alisema, watu watakaoruhusiwa kuingia nchini humo ni wale wanaotoa huduma muhimu,watu wanaorudishwa Malawi, na waliosafiri kwa shughuli za kibiashara.

Chiponda pia alisisitiza kuwa mikusanyiko ya umma itaruhusiwa kwa watu wasiozidi 100, huku washiriki wakitakiwa kufuata kwa makini kanuni za udhibiti wa virusi vya Corona.