LONDON, England
MANCHESTER City imefanikiwa kwenda nusu fainali ya Kombe la Ligi baada ya ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.

Magoli ya ManCity yalifungwa na Gabriel Jesus kunako dakika ya tatu, Riyard Mahrez (dk. ya 54), Phil Foden (dk. ya 59) na Aymeric Laporte (dk. ya 73). Goli la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Alexandre Lacazette kwenye dakika ya 31.

Matokeo ya mechi nyengine ya robo fainali ya Kombe la Carabao, Brentford iliichapa Newcastle United 1-0 kwenye uwanja wa Brentford Community. Bao pekee lilifungwa na Joshua da Silva kunako dakika ya 66.

Michuano hiyo ilitarajiwa kuendelea jana kwa Stoke City na Tottenham Hotspur kwenye uwanja wa uwanja wa Bet365 na Everton dhidi ya Manchester United katika dimba la Goodison Park.(BBC Sports).