LONDON, England

SADIO Mane, nyota wa klabu ya Liverpool raia wa Senegal alifikisha bao lake la 6 ndani ya Ligi Kuu England, wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya West Brom.

Wakiwa Uwanja wa Anfield Mabingwa hao watetezi waliruhusu bao dakika za lala salama kwa kuwa walianza kushinda mapema kipindi cha kwanza.

Bao la Mane ambaye ambaye yupo nafasi ya pili kwa utupiaji ndani ya Liverpool kinara akiwa ni Mohamed Salah mwenye mabao 13, lilipachikwa dakika ya 12 na lile la West Brom lilipachikwa na Semi Ajayi dakika ya 82.

Sare hiyo unaifanya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi kuongeza pointi moja na kufikisha jumla ya pointi 32 nafasi ya kwanza huku West Brom ikiwa nafasi ya 19 .