NA MARYAM HASSAN

MASHEHA wa Wilaya ya Mjini, wamemuomba Waziri wa Ardhi Maendeleo na Makaazi kupitia shirika la Nyumba kuwapatiwa orodha kamili za nyumba za serikali pamoja na umiliki wao, ili kuweza kurahisisha utendaji wa kazi zao.

Wakizungumza katika kikao na Waziri wa Wizara hiyo, huko katika ukumbi wa Wizara hiyo, walisema, kupatiwa kwa hati hizo zitasaidia kuwajua wakaazi wa nyumba hizo pamoja na wadaiwa sugu ambao wanaishi katika nyumba hizo.

Wamesema katika  kufuatilia nyumba hizo wamebaini  kuwa katika nyumba hizo kunachangamoto nyingi zikiwemo mmiliki  halali wanaoishi katika nyumba  na kukodisha.

Sheha wa shehia ya Miembeni, Ali Abdallah Kidemere, alisema katika nyumba anazozisimamia zilizokuwepo katika shehia zao wapo wanaoishi ambao utaratibu umefuatwa na wapo wanaoishi nyumba za serikali.

Alisema ni vyema pia kufanyiwa marekebisho wa mkataba wa nyumba hizo,  kwani kumekuwepo tatizo kwa watu waliopewa nyumba kwa waliovunjiwa na hawajapewa hati jambo ambalo limekuwa likiengeza tatizo katika nyumba hiyo.

“Katika nyumba hizi tumebaini watu wanaishi ni tofauti na mikataba tuliokuwa nayo sie na wengine wanaishi bure bila ya kuchangia kodi zinazotolewa katika Shirika la Nyumba” alisema.

Hata hivyo, alisema kuwa Masheha kwa sasa wamekuwa muhanga kwani  watendaji wa Shirika la Nyumba hawaonani na Masheha hadi wakati wakiwa na shida zao huwatambua masheha hao.

Sambamba na hayo, waliahidi kuendelea kufanya nae kazi bega kea bega, ili kuona kazi zinakuwa kwa urahisi na kuendana na Kasi ya Rais wa Zanzibar katika kuona kila mwananchi anayestahiki kulipa kodi analipa kwa wakati uliopangwa.

Sambamba na hayo, walisema kuwa katika hizo kumekuwa na changamoto ya miundombinu mibovu ikiwemo karo Jambo ambalo linafanya uwepo wa uchafu na kuzagaa taka.

 Nae Waziri wa Wizara hiyo, Riziki Pembe Juma, amewahakikishia Masheha hao kuwa na mashirikiano ya pamoja, ili kuhakikisha changamoto za nyumba hizo za maendeleo  zinatatuliwa  pamoja na wakaazi kulipa madeni.

Alisema  kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi wanaotafuta nyumba za serikali  kutozwa kilemba, hali ambayo  inawapa ugumu kuzipata nyumba hizo.

Sambamba na hayo, alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto na kuahidi kuzitatua changamoto hizo ili maendeleo ya nyumba hizo zifikiwe.