NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Matulanga, amesema atahakikisha anasimama vyema masuala ya maendeleo ya jiji hilo, ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Pia ameliomba baraza la Madiwani kufanya kazi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele kwa kufanya hivyo wataleta ufanisi , pamoja na kutenda haki kwa wananchi .
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kula kiapo madiwani 21, katika jiji hilo pamoja na ufunguzi wa kikoa cha kwanza cha baraza ambapo alisisitiza madiwani hao kwenda kufanya kazi kwa mashirikiano makubwa ili kuleta mendeleo .
“Tukifanya kazi kwa mashirikiano makubwa naimani tutapata maendeleo katika jiji letu la Dar es Salaam” alisema.
Aidha alisema baraza hilo kwa pamoja liende kusimamia vyema majukumu yao na kushiriki vikao watakavyoita ili kuleta ufanisi na kuleta maendeleo katika jiji hilo.
Sambamba na hilo, alisema kamati tano zimeundwa ndani ya baraza hilo ikiwemo ya Fedha na Uongozi ,Kamati ya Mipango na Uratibu, Kamati ya Mipango miji , Mazingira na Miundombinu, Kamati ya Huduma za Kijamii, Kamati ya Usalama na Maadili ya Madiwani, ili kwenda kusimamia majukumu mbali mbali katika maeneo yao husika.
Hata hivyo, zoezi la uapishwaji wa Madiwani 21 limekamilika katika Jiji la Dar es Salaam ambapo waliapishwa na hakim Mkazi wa Mahakama ya Sokoine Drive ya jiji, Anifa Mwingira.