NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Kagera Sugar, Yusuph Mhilu, amewapa tahadhari wapinzani wao Polisi Tanzania kuelekea kwenye mchezo wao wa leo ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera ambapo katika mchezo uliopita Kagera Sugar walipokea kichapo cha mabao 2 – 1 dhidi ya Ihefu FC.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana kwa njia ya simu, Mhilu alisema kwamba hajacheza muda mrefu kwa hiyo kama leo atapata nafasi atahakikisha anafunga.

Alisema Polisi walitoka sare na wao walipoteza mchezo uliopita jambo linalopelekea kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa kuwa kila timu inavutia upande wake na inahitaji kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kupata matokeo mazuri.