NA VICTORIA GODFREY

SHIRIKISHO la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) linatarajia kufanya mkutano mkuu leo Msasani Beach, Dar es Salaam.

Akizungumza na Zanzibarleo, Katibu Mkuu wa TAWF,Abraham Nkabuka, alisema lengo la mkutano huo ni kupitia ajenda mbalimbali.

Alisema baadhi ya ajenda ni kupitia taarifa ya mwaka ya maendeleo na fedha.

Alisema mkutano huo utapitia majina ya wachezaji waliochaguliwa kwenye mashindano ya klabu bingwa Taifa iliyofanyika mwezi huu jijini Arusha, kwa ajili ya kuwaandaa kwa mashindano ya kimataifa yatakayofanyika mwaka ujao.

Nkabuka alisema  pia wataupitia mpango Mkakati kuweza kuuimarisha kabla ya kuupeleka Baraza la Taifa la Michezo (BMT) kesho kutwa.