NA MOHAMED HAKIM
TIMU ya soka ya Vijana Wilaya ya Mjini U-17 inayoshiriki mashindano ya Watoto Mapinduzi cup imepania kunyakua kombe la michuano hiyo kwa mara ya nne mfululizo.


Akizungumza na muandishi wa habari hizi kocha wa timu hiyo, Mohamed Ali Mohamed (Xavi) alisema timu yake imejipanga vizuri kila idara na wanasubiri kwa hamu kubwa kujua nani watapangiwa nae katika hatua ya robo fainali.


Alisema mpaka kufikia hatua ya robo fainali walifanya kazi kubwa kwani kundi lao lilikuwa gumu kutokana na upinzani ulikuwepo na wilaya Kati pamoja na wilaya ya Kaskazini A, pia baadhi ya timu zilikuwa zinafanya udanganyifu kwa kuchezesha wachezaji waliozidi umri.


“Licha ya baadhi ya wilaya kufanya udanganyifu kwa kuingiza wachezaji wenye umri mkubwa, bado tumeweza kuzifunga na hii kutokana na ubora wa timu yetu, naamini nitalitetea taji na kuweka heshima kwa wilaya yetu ya Mjini.” Alisema Xavi


Timu ya wilaya ya mjini imefuzu hatua ya makundi baada ya kuifunga timu ya Wilaya ya Kaskazini A bao 1-0 na kutinga robo fainali.