NA MWANAJUMA MMANGA
MRADI wa soko la samaki Malindi unatarajia kuendelea tena ujenzi huo ifikapo mwezi wa April mwakani 2021baada ya kusita ujenzi huo kutokana na janga la Corona.
Mratibu wa mradi huo, Daudi Haji Pandu, kutoka Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko ofisini kwake Maruhubi Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja.
Alisema mradi huo unajengwa chini ya ufadhili wa kampuni ya JECA kutoka Japan kwa ajili ya kuendelea na ujenzi huo ambae pia ni mkandarasi.
Alisema wakati janga la corona lilipoanza serikali ya Japan iliwataka raia wake kurudi nchini kwao, na hadi sasa hawajaruhusiwa kutokana bado janga hilo kuendelea hadi leo.
Alisema wanategemea ujenzi huu kuendelea mwezi wa nne na matarajio yao mkandarasi huyo kurudi kipindi hicho kwa ajili ya kuanza ujenzi huo katika sehemu walioiacha.
“Tunachomsubiri hivi sasa ni mfadhili tu ni taasisi ya JECA kutoka Japan kwa ajili ya kuendelea na ujenzi huo.
Alisema kazi inayofuata ni ujenzi wa jingo la ofisi na sehemu ya kufanyia biashara wa mnada wa samaki.
Alisema kazi kuwa tayari hatua kubwa iliyofikiwa ya mradi huo ikiwemo uwekaji wa nguzo za banda la kupumzikia wafanyabiashra wa soko hilo umeshakamilika pamoja na uzikaji wa vyuma kwa ajili ya kuzuia maji pamoja na uwekaji sakafu.
Alisema ujenzi huo umegawika katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwaza utahusisha ujenzi wa soko ambao utajumuisha eneo la ofisi, kuuzia samaki, sehemu ya kuhifadhia nyavu, jenereta na chumba cha baridi na sehemu ya pili ni ujenzi wa bandari ya uvuvi ya kisasa ( diko) ambayo itahudumia boti mbali mbali za wavuvi wa Zanzibar.
Alisema mradi huo unatarajiwa endapo utakamilika utagharimu Dola za Kimarekani milioni 9,291,176 ambapo mradi huo endapo utamalizika utaweza kusaidia kuwawezesha wadau wanaotumia diko la la malindi kuuzia na kununulia samaki wao wakiwa salama kiafya.
Alisema pia mazingira mazuri ya kuwekea vyombo vya wavuvi na biashara kwa wavuvi na wachukuzi, madalali, wauzaji wadogo wadogo na wanunuzi.
Alisema matarajio ya soko hilo litakapomalizika litaweza kutoa ajira kwa wafanyabiashara 6,500 watatumia eneo hilo na zaidi ya wananchi 6,000 wa zanzibar watafaidika na mradi huo moja kwa moja na zaidi ya wazanzibar laki tisa watafaidika na mradi huo.
Alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikia mradi huo, hivyo amewashauri wananchi na wavuvi walioupisha ujenzi huo kuendelea kuwa wastahamilivu na kuendelea kutoa msaada pale ambapo inapohitajika.