Aling’ara Ujamaa na Zanzibar Heroes

Ashauri uendelezaji soka ya vijana

NA ABOUD MAHMOUD
UJAMAA ni moja ya klabu maarufu visiwani Zanzibar ambayo imeweza kujizolea sifa kutokana na uwezo waliokuwa nao wachezaji wake katika mchezo wa soka.
Takriban miaka kadhaa kuanzia mwaka 1960 timu hiyo ilionesha umahiri wa soka na kuvutia wachezaji wengi kutoka mitaa mbali mbali kujiunga nayo.

Kama utataja majina ya timu mbali mbali za mchezo huo visiwani hapa bila ya kuitaja Ujamaa, utakua hujaitendea haki kutokana na uimara uliokuwa nao.
Mbali na hilo, Ujamaa ambayo makao makuu yake yapo katika mtaa wa Rahaleo iliwahi kukusanya wachezaji wengi ambao hivi sasa ni watu maarufu na viongozi katika nchi hii.

Miongoni mwa watu maarufu hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Lakini miongoni mwa wachezaji waliochezea klabu hiyo ni pamoja na Mussa Khamis Baucha ambae naye aliong’ara akiwa na Ujamaa na timu ya taifa ya Zanzibar kwa miaka kadhaa.

Mwandishi wa makala hii aliweza kumtafuta mwanasoka huyo ambae kwa sasa anaishi nchini Denmark na kukutana nae huko nyumbani kwake katika mtaa wa Malindi mjini Unguja na kumuelezea kwa kina mambo mbali mbali katika ulimwengu wa soka.

Mahojiano hayo ambayo yalikwenda kama hivi:- Naomba kujua historia yako kwa ufupi, umezaliwa mwaka gani na wapi?

“Jina langu naitwa Mussa Khamis ‘Baucha’, nimezaliwa Februari 11 mwaka 1947 huko Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja nikiwa mtoto wa tano katika familia ya watoto 11”.

Elimu yako ulianza kuipata mwaka gani na wapi?
“Nilianza masomo nikiwa na umri wa miaka sita katika skuli iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Gulioni wakati huo ilikua ni Quraan Class, baadae nikaendelea hapo hapo na elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka la nane nilipomaliza mwaka 1961 na sikuendelea tena na masomo ya skuli, nilijiendeleza mimi mwenyewe tu,”.
Kuhusu soka ulianzia vipi?

“Soka nilianza tangu nikiwa mdogo wakati huo nasoma skuli kulikua na timu ambayo ilikua ya wanafunzi na mimi nikajiunga nikiwa na wenzangu akina Enzi Talib, Zubeir Abdallah,Kitwana Rajab na wengine wengi,”.

Ilikuaje mpaka ukajiunga na Ujamaa wakati wewe nyumbani ni Malindi?
“Ni kweli nyumbani Malindi, lakini, mimi nilijiunga na timu hiyo wakati huo inaitwa Wolvehampton kutokana na ushawishi nilioupata kwa wanafunzi wenzangu niliokuwa nasoma nao skuli, wengi walikua wanaichezea timu hiyo,”.

“Wakati huo nacheza Wolvehampton, nilikuwa nasoma skuli baada ya kutoka matokeo na nilikua nimefeli kwa kweli niliudhika na ndipo nikaamua kuachana na soka ”.

Ilikuaje mpaka ukaamua kurudi tena uwanjani?
“Baada ya kuacha kucheza mpira, mwalimu wetu wa soka marehemu Hassan Mzibondo alikuja nyumbani kuzungumza na mimi pamoja na baba angu ili nirudi nikacheze mpira hivyo nikaona wazee wangu wawili washanikalia usoni wananambia maneno hayo nikaona bora nisiwavunje na nirudi uwanjani,”
Uliporudi ulikua unacheza nafasi gani?
“Niliporudi nilikua nacheza beki wa kulia nikicheza nambari mbli wakati huo nilikua nachezea timu ndogo daraja la Juvenile katika timu hiyo hiyo ya Wolvhampton,”.Uliwahi kucheza timu kubwa katika kikosi hicho?

“Ndio nilicheza timu kubwa,nakumbuka mwaka 1964 tulianza kucheza timu kubwa na wachezaji wengine waliongezeka akiwemo Ali Tali, Saleh Boss, Shaaban Lalo, Abdallah Karang’anda, Said Waziri, Yussuf Ramadhani na wengine wengi,”.
Ilikuaje mpaka ukaamua kurudi tena uwanjani?

“Baada ya kuacha kucheza mpira, mwalimu wetu wa soka marehemu Hassan Mzibondo alikuja nyumbani kuzungumza na mimi pamoja na baba angu ili nirudi nikacheze mpira hivyo nikaona wazee wangu wawili washanikalia usoni wananambia maneno hayo nikaona bora nisiwavunje na nirudi uwanjani,”
Uliporudi ulikua unacheza nafasi gani?

“Niliporudi nilikua nacheza beki wa kulia nikicheza nambari mbli wakati huo nilikua nachezea timu ndogo daraja la Juvenile katika timu hiyo hiyo ya Wolvhampton,”.

Uliwahi kucheza timu kubwa katika kikosi hicho?
“Ndio nilicheza timu kubwa,nakumbuka mwaka 1964 tulianza kucheza timu kubwa na wachezaji wengine waliongezeka akiwemo Ali Tali, Saleh Boss, Shaaban Lalo, Abdallah Karang’anda, Said Wazir, Yussuf Ramadhani na wengine wengi,”.
Baada ya hapo mliendelea vipi na Wolvehampton?

“Mwaka 1966 hapo ndipo ilipozaliwa rasmi Ujamaa na jina la Wolvhampton lilipomalizika na mwaka huo huo nikiwa na Ujamaa nikabahatika kuchaguliwa katika kikosi cha taifa ya Zanzibar”.

Ukiwa ndani ya timu ya taifa unakumbuka uliungana na wachezaji gani?
“Wengine alikuwa Abdulmajham, Ramadhan Katembo,Mzee Kheri,Suleiman Nyanga,Salhina Maftah,Mzee Boti, Shafi Mussa, Rashid Ubwa na wengine, lakini, wengine tayari washafika mbele ya haki, allwah awasemehe makosa yao,”.
Timu ya taifa mlikua mnashiriki mashindano gani?

“Wakati huo kulikua na mashindano ya Afrika Mashariki ambapo nchi zilizokua zikishiriki ni pamoja na Tanzania Bara,Tanzania Visiwani,Kenya na Uganda,”.
Mlipokua mnashiriki mashindano hayo je mliwahi kuchukua ubingwa?

“Nisiwe muongo hatujawahi kuchukua ubingwa hata mara moja tulikua tunaenda lakini mwisho tunatolewa na pia nilidumu na timu ya taifa mpaka mwaka 1970 hapo nikaacha kuchaguliwa timu ya taifa na kubaki Ujamaa,”.
Mwaka gani uliacha kucheza soka na sababu ilikua nini?

“Ilipofika mwaka 1976 nikaamua rasmi kuacha kucheza mpira na sababu kubwa zilizonifanya niache ni kupitwa na umri na kiwango cha soka kilikua hakipo tena, nikaamua niondoke niwaachie vijana”.

Kuna mechi gani ambayo hutoisahau maisha yako?
“Siwezi kusahau mechi ambayo tulicheza na timu ya Navy, mpaka tunamaliza kipindi cha mwanzo tulikua tupo sare ya goli 1-1, lakini, baadae karibu mchezo kumaliza tuliongezwa goli, ilituuma sana,”.

Wakati ulipokua ukicheza kabumbu ulikua unavutiwa na mchezaji gani?
“Wachezaji wawili walionivutia ni marehemu Abdulmajham na Suleiman Nyanga, nilikua napenda kuwaangalia wanavyocheza mpira,”.

Kwanini ulienda kucheza soka mbali na kuacha timu ya nyumbani?
“Wanafunzi niliosoma nao wengi walikuwa wanacheza Ujamaa na hao ndio walionishawishi nijiunge na klabu ile jengine pia lililonifanya nisihame Ujamaa ilikua timu haina ubaguzi wachezaji wa mitaa mbali mbali walichezea klabu ile,”.
“Nilipata tabu kwanini nisicheze Malindi nikaenda kucheza Ujamaa, nilikua natupiwa maneno, nanuniwa na hata wakati mwengine nilikua nakwenda kununua bokoboko siuziwi”.

Kwa soka la Ulaya unapendelea timu gani na sababu gani?
“Mimi shabiki mkubwa wa Arsenal ya England na sababu za kuifanya niipende klabu hiyo kutokana na uzalendo waliokuwa nao, wanakuza vipaji vya wachezaji wana timu kubwa na ndogo na mchezaji akiwa mkubwa analetwa timu kubwa hii inasaidia kuondosha gharama za kununu wachezaji,”.

Baada ya kuhamia Denmark ulikua unacheza soka?
“Hapana sikuwa mchezaji kwa sababu nilipoondoka hapa nilikua nishastaafu kucheza alafu nilipofika kule nikaendelea kufanya kazi nyengine kwahiyo sikutaka kujiingiza kwenye soka,”.

Tofauti gani unayoitoa baina ya soka la zamani na sasa hivi?
“Tofauti ipo kubwa mpira wa zamani tulikua tunacheza kwa ari na tunaumwa na timu zetu na tulikua hatulipwi kitu chochote,tofauti na sasa hivi wachezaji wanalipwa pesa nyingi lakini hawana ari wala mapenzi na vilabu vyao,”
Una ushauri gani kwa serikali kuhusiana na mchezo wa soka“Ushauri wangu kwa serikali ihakikishe kila siku inazidi kukuza elimu ya soka hasa kwa upande wa walimu, kufanya hivyo itasaidia soka letu kukuwa kama nchi za wenzetu,”.

Kwa upande wa wachezaji wa zamani unawashauri nini?
“Naishauri ZFF kuwatumia wachezaji wa zamani katika kukuza soka letu naamini wanajua mambo mengi kwa hiyo ni vyema kuwatumia ,”alisema.Mussa Khamis Baucha baba mwenye familia ya watoto watatu amesema katika watoto wake hakuna aliyemrithi katika mchezo wa soka na yeye hakurithi kwa mzee wake .