ALGIERS, Algeria
MIAMBA ya Ligi ya Kuu ya Italia ‘Serie A’ ya Napoli haitamuuza beki wa kushoto wa Algeria, Faouzi Ghoulam, katika dirisha la uhamisho la Januari.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mzaliwa wa Ufaransa ameshuhudia miaka mitatu iliyopita ya kazi yake ikiharibiwa kutokana na maumivu, akianza na kupasuka mguu wake katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City mnamo Novemba 2017.

Amecheza mara nne kwenye ‘Serie A’ msimu huu, na ameonekana katika michezo 40 tu ya ligi tangu kuanza kwa kampeni ya 2017-18.Huku Ghoulam akiwa anajiandaa kuingia miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake na Napoli na kutimiza miaka 30 katika wiki za mwanzo za 2021, uvumi umekuwa mwingi kwamba mchezaji huyo wa Algeria anaweza kuuzwa katika dirisha lijalo la uhamisho wa Januari.

Hata hivyo, ripoti za vyombo vya habari vya Italia, pamoja na zile za ‘Corriere dello Sport’, zinasisitiza kwamba meneja wa Napoli, Gennaro Gattuso anataka kumuweka Ghoulam kwenye kikosi, kwani anaweza kudhihirisha mchezaji muhimu katika miezi mingi ijayo.(Goal).