MANAGUA, NICARAGUA
 BUNGE la Nicaragua limepitisha sheria mpya inayowazuia watu ambao serikali inaamini walifadhili majaribio ya kumuondoa Rais Daniel Ortega au kuchochea kuwekewa vikwazo vya kimataifa maofisa wake kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa 2021.

Sheria hiyo mpya iliungwa mkono na wabunge 70 kutoka chama cha Ortega cha Sandinistas, kwenye bunge lenye viti 92.

Wakosoaji wa serikali ya Nicaragua walisema sheria hiyo inajaribu kuwatisha wapinzani wa Ortega ambaye mwakani atagombea muhula wa tatu madarakani.

Serikali ya Ortega inaushutumu upinzani kwa kujaribu kufanya mapinduzi, na kuchochea kuwekewa vikwazo vya kimataifa maofisa wake baada ya kuibuka maandamano ya kuipinga serikali Aprili 2018.