Alikuwa ajenti muaminifu wa CIA
Uzawa wake umejaa mazonge
MANUEL Antonio Noriega Moreno alikuwa kiongozi wa kijeshi aliyeitawala nchini ya Panama nchi iliyoko Marekani ya Kusini, lakini hutumiwa kama njia kuu ya kuingia na kutoka Amerika ya Kusini.
Noriega ambaye alikuwa akichukuliwa kama miongoni mwa marais dikteta waliowahi kutawala hapa ulimwenguni, alizaliwa Februari 11 mwaka 1934 ambapo muda wa uhai wake wa miaka 83, ulimalizika Mei 29 mwaka 2017.
Mtawala huyo wa kijeshi, aliliongoza taifa hilo kwa msaada mkubwa wa Marekani kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1989, kabla ya maswahibu zake wamarekani walipovamia nchi hiyo kijeshi na kumng’oa madarakani.
Noriega alikuwa kupenzi cha tona nkutoke cha Marekani, akilfanyia kazi shirika la ujasusi la nchi hiyo CIA, lakini cha kungazwa rafiki huyo ndiye aliyemgeuka na kumuondoa madarakani.
Alizaliwa jijini Panama na kusoma katika moja ya skuli za kijeshi mjini Lima na baada ya hapo ya sekondari ya Americans, baadae alipata fursa ya kujiunga na jeshi la Panama.
Akiwa jeshini alipanda ngazi za uofisa taratibu na kuwa mmoja wa maafisa wa jeshi, ambapo alifanya kazi kwa karibu na mkuu wa idara ya keshi ya intelijensia wa jeshi la nchi hiyo Omar Torrijo.
Baada ya Omar Torrijo ambaye ndiye aliyekua mkuu wa intelijensia wa jeshi kufanya la Panama kufanikiwa katika jaribio la mapinduzi, hivyo Noriega akakabidhiwa yeye jukumu la kuiongoza idara hiyo mwaka 1968.
Kufuatia kifo cha Torrijo mwaka 1981, Norriega akajiimarisha kiutawala mpaka akawa kiongozi wa Panama, ingawa sio rasmi mwaka 1983 (de facto ruler of panama).
Historia inaonesha kuwa kuanzia mwaka 1950 mpaka karibu na kipindi ambacho Marekani walikuja kumvamia na kumuondoa madarakani, Norriega alikua akifanya kazi kwa karibu sana na shirika la ujasusi la Marekani CIA.
Norriega alikua moja ya vyanzo muhimu vya kuamnika vya CIA, hasa kwenye masuala ya intelijensia, pia ilikua ndio sehemu muhimu ya kuanzishia, kupanga pamoja na kupitishia silaha na fedha linapokuja suala la operasheni yoyote inayohusu masuala ya kijeshi kati ya Marekani ya Kati na Kusini.
Dikteta huyo, pia alijihusisha na biashara ya dawa za kulevya hasa ‘cocaine’ kwa kiwango cha hali ya juu kitu ambacho wamarekani walikifahamu fika kwa miaka mingi.
Pamoja na Marekani kufahamu biashara ya unga iliyokuwa ikifanywa na Noriega, ilimuachilia aendelee na biashara hiyo, kwani bado alikuwa ana umuhimu wa kipekee katika kulipatia taarifa za kuaminika za kiitelijensia zenye maslahi na Marekani, shirika la ujasui la CIA.
Aidha Marekani pia ilimfumbia macho Noriega aendelee kufanya biahsara hiyo kutokana na umuhimu wake hasa kwenye masuala ya kijeshi la kiusalama katika ukanda huo wa Marekani ya kati na kusini.
Utawala wa Norriega nchini Panama, uligubikwa na ukandamizwaji wa vyombo vya habari, uimarishwaji wa jeshi, pamoja na uteswaji na ukandamizwaji wa mahasimu wa kisiasa.
Noriega aliweza kusimamia uchaguzi wowote na kupata matokeo anayotaka yeye, alijitengenezea utajiri mkubwa kupitia biashara yake ya dawa za kulevya.
Taratibu mahusiano na urafiki wake wa dam dam na Marekani ulianza kupungua kwa sababu ya vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wananchi wake, lakini jengine lililokera zaidi ni hatua ya Noriega kuanza kuuza taarifa za kiintelijensia kwa mahasimu wa Marekani.
Mwaka 1988 Norriega aliwekwa kwenye orodha ya matajiri wakubwa wenye kusafirisha dawa za kulevya na kuziingiza nchini Marekani kupitia mwambao wa Miami huko Florida.
Marekani haikuwa na jinsi ililazimika kuivamia Panama mwaka 1989 na kumuondoa madarakani, ambapo ilimchukua dikteta huyo hadi Marekani ambako alipandishwa mahakamani.
Noriega alisomewa makosa manane yanayohusiana na kuuza dawa za kulevya kupanga na kusafirisha dawa ya kulevya na utakatishaji wa fedha haramu, ambapo mwaka 1992 alihukumia kifungo cha miaka 40 jela kilichopunguzwa kuwa miaka 30 jela.
Kifungo cha Norriega nchini Marekani kilisitishwa mwaka 2007 baada ya nchi ya Panama pamoja na Ufaransa kuomba kumuhukumu bila yeye mwenyewe kuwapo mahakamani kwa mauaji mwaka 1995 na utakatishaji wa fedha mwaka 1999.
Ufaransa ilikabidhiwa mtuhumiwa huyu mwaka 2010 mwezi wa Aprili baada ya ombi lao kukubaliwa na alifikishwa Paris Aprili 27 mwaka 2010 na baada ya kesi yake kusikilizwa upya, ambapo mwezi Julai mwaka 2010 alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Makubaliano ya kumhamisha gereza kutoka Ufaransa na kumpeleka Panama kutumikia kifungo cha miaka 20 yalifikiwa ikiwa ni vifungo vyote vilivyomkabili nchini Marekani na Ufaransa, hivyo alipelekwa Septemba 23 mwaka 2011 alisafirishwa hadi nchini Panama.
Norriega alifariki katika hospitali ya Santo Thomas nchini Panama Mei 29 mwaka 2017, ikiwa ni miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji ili kuzuia kuvuja damu katika ubongo.
Noriega alizaliwa Panama, katika familia ya kimasikini ya mchanganyiko wa rangi ambayo inajumuisha wazawa wa marekani, waafrika na waspaniola.
Mama yake anazungumziwa kuwa mpishi na dobi na baba yake alikua muhasibu na hakuishi muda mrefu na mama yake alifariki kwa maradhi ya kifua kikuu wakati Noriega akiwa mdogo.

Noriega alilelewa na bibi yake katika nyumba ya chumba kimoja katika makaazi ya watu wengi za mji wa Terraplen. Waandishi wa habari na wa vitabu wanasema kwamba sio mtoto halali wa Ricaurte Noriega bali ni mtoto wa ‘house boy’ wao ambaye inasadikiwa alitembea na mama mwenye nyumba, ‘houseboy’ huyo alijulikana kwa jina la Moreno.
Norriega alipata elimu yake ya mwanzo Escuela República de México, na baadae katika skuli ya sekondari inayoheshimika sana jijini Panama kwa kuzalisha wanamapinduzi wengi na viongozi wa kisiasa ya Instituto Nacional.
Akiwa katika skuli hizo alikua anaelezewa kama kijana ambaye yuko makini muda wote. Pia anaelezewa kama kijana aliyependa sana kusoma na alikua anavishwa vizuri na mlezi wake.
Wakati akiwa Instituto Nacional, alikutana na kaka yake luis ambaye alikua mwanaharakati katika skuli hiyo, Norriega kabla ya hapo hakuwahi kukutana na ndugu wa kuzaliwa kwa upande wowote sio mama wala baba.
Huyu Luis ndiye hasa alimleta Norriega kwenye siasa na kumpeleka kwenye chama cha kijamaa upande wa vijana. Kuna wakati alikua akiishi pamoja na kaka yake.
Wakati akiwa katika chama hicho upande wa vijana alishiriki katika maandamano na pia kuandika baadhi ya makala ya kukosoa uwepo wa Marekani katika Panama.
Katika wakati huo ndio inasadikiwa kwamba ndipo wamerekani walimchukua katika kitengo chao cha intelijensia na alikua akitumika katika kuwapa taarifa wamarekani za kikundi cha wanaharakati wenzake akiwemo kaka yake.
Aliendelea kufanya kazi na wamerekani katika sehemu mbalimbali mpaka mwaka 1980 na inasadikiwa aliwahi kulipwa na aliendelea kulipwa kwa mda mrefu kwa kutoa taarifa hizo.
Baada ya kumaliza katika skuli ya Instituto Nacional alipata scholarship kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Chorrillos Military School kilichopo nchini Peru mjini Lima kwa kusaidiana na Luis ambaye tayari alikua anafanya kazi katika ubalozi wa panama nchini Peru.
Alikua na ndoto zilizoota mbawa za kuwa daktari ila alishindwa kupata nafasi katika chuo kikuu cha Panama. Akiwa nchini Peru alitengeneza urafiki na Roberto Díaz Herrera, ambaye baadae alikuja kuwa rafiki wa karibu na muhimu sana.
Norriega baadae alioana na Felicidad Sieiro de Noriega, ambaye walikutana mwaka 1960 na walifanikiwa kupata mabinti watatu ambao ni Lorena, Sandra na Thays Noriega.
Siero alikua ni mwalimu wa skuli na Norriega alikua mwanajeshi, familia ya mkewe Norriega haikufurahishwa na ndoa hiyo, pamoja na hayo Norriega anaonekana hakuwa na utulivu katika ndoa yao na mara kadhaa mkewe alisikika akitaka ndoa hiyo ivunjwe ingawaje baadae alibadili mawazo na kuendelee na mumewe.
Wahusika hawa wanne wa familia hii ya Norriega wanaripotiwa kwamba walikuwepo wazima wa afya wakati wa kifo cha Norriega.