NAIROBI, Kenya

ROBERT OKONG’O ameshinda mashindano ya wazi ya kila mwaka ya Jumuiya ya Gofu ya Sunset yaliyofanyika kwenye klabu ya uwanja wa Gofu ya Nyanza nchini Kenya, yaliyovutia wachezaji zaidi ya 150.

Okong’o alipata pointi 40 za kufunga, akimaliza mikwaju mitano, na kuwaacha Charles Handa aliyepata pointi 38, na mikwaju 17 kwenye mashimo sita ya mwisho. Handa alikuwa mshindi wa pili bora kwa jumla.

Joram ocholla aliibuka mshindi wa tatu kwa pointi 38 na mikwaju 28 na kufuatiwa na Ojwang Lusi, katibu wa zamani wa Kaunti ya Kisumu, ambaye alikuwa wa nne kwa pointi  37 kutokana na mikwaju 16.

 Okong’o amesema mwaka kesho jumuiya yake ya Robert O Foundation, itaendelea kukuza mashindano ya gofu na atafadhili michezo zaidi kama hiyo kwa ajili ya mwaka kesho.