TOKYO, Japan

MCHEZAJI wa timu ya Harambee stars ya Kenya Michael Olunga, amefurahia msimu huu akiwa klabu ya Kashiwa Reysol kwenye Ligi ya daraja la kwanza ya Japan J1.

 Olunga amefunga mabao 28 na kumaliza akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo, mchezaji anayemfuatia amemuacha kwa jumla ya magoli manane.

Mafanikio hayo pia yamemfanya achaguliwe kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi kwenye ligi hiyo kwa mwaka 2020.

Magoli aliyofunga ni karibu nusu ya magoli 60 yaliyofungwa na klabu yake ya Kashiwa Reysol katika msimu uliopita, lakini bahati mbaya timu yake ilimaliza ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 52.

Akizungumzia mafanikio hayo, kijana huyo mwenye miaka 26 aliwashukuru wachezaji wenzake, klabu na mashabiki kwa kumsaidia kufikia hatua hiyo.