PARIS, Ufaransa

IMERIPOTIWA kuwa Mauricio Pochettino amesaini mkataba mpya wa kuwa kocha wa klabu ya Paris Saint-Germain,(PSG) inayoshiriki Ligue 1.

Mwandishi mkongwe nchini Italia wa masuala ya michezo, Fabrizio Romano amesema bosi huyo wa zamani wa klabu ya Spurs amesaini dili jipya Jumapili Disemba 27.

Pochettino anakuwa mrithi wa mikoba ya kocha wa zamani wa PSG, Thomas Tuchel ambaye alifutwa kazi kwa makubaliano na timu hiyo kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo. 

Tuchel alifutwa kazi muda mchache akitoka kuongoza kikosi chake kushinda mabao 4-0 dhidi ya  Racing Strasbourg.

Pochettino amekuwa nje kwa muda mrefu bila kuwa na timu baada ya kufutwa kazi ndani ya klabu ya Spurs mwaka uliopita na amekuwa akihusishwa kujiunga na timu mbalimbai ikiwa ni pamoja na Barcelona, Manchester United na Real Madrid.