HUSNA SHEHA NA MWANAJUMA MMANGA
JESHI la polisi Mkoa wa Kusini Unguja, limeandaa mpango mikakati wa kuhakikisha sikukuu ya krismasi inafanyika kwa amani na utulivu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Suleiman Hassan Suleiman, aliyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofisini kwake Tunguu.
alisema wamejipanga kuweka askari wa usalama wa barabarani katika maeneo yote ili kuimarisha usalama barabarani na katika maeneo yote ya wilaya hiyo.
Alisema ili kudhibiti gari na vespa na vyombo vyengine zinazokwenda mwendo kasi ili kuepusha ajali zisizokuwa za ulazima.
“Kumekuwa na tabia ya kipindi cha skukuu gari nyingi zinakimbilia abiria na kwenda mwengo kasi jamboambalo linapelekea kutokea kwa ajali na kusababisha ulemavu wa watu na wengine vifo,” alisema Kamanda Suleiman.
Alisema iwapo madereva watakwenda mwendo wa wastani hata pale ambapo inapotokezea bahati mbaya na ajali inapotokezea inaweza madhara ikawa madogo.
Alisema kwa upande wa mitaani waliko jamii jeshi hilo limepanga kufanya doria mbali mbali kuhakikisha maeneo yote ya mkoa huo kuwa salama pamoja na kulinda raia na mali zao.
Aidha alisema pia watahakikisha katika sehemu za ibada ya waumini wa dini za kikiristo watakuwepo wataweza kutoa ulinzi kwa maeneo hao pia watazidisha doria ili kuhakikisha maeneo hayo wanasali kwa amani na usalama.
Pia watafanya doria katika maeneo ya mahoteli ya mkoa huo ili kuona sehemu hizo zinakuwa salama na amani katika kipindi chote hicho hasa maneeo ya fukwe wa bahari.
Aliongeza kusema kuwa kunakuwa na tabia ya watoto kuvishwa vitu vya thamani wakati wanapokwenda kusheherekea skukuu ama katika ibada hivyo kutowava sambamba na hilo wazazi kuwatilia namba katika mifuko ili pale watapopotea bkuweza kuwasiliana na wazee wao iwe rahisi.
Kwa upande wa mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamanda wa Polisi mkoani humo Haji Abdalla Haji alisema wamejipanga vyema na kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mkoa huo kwa kipindi chote cha sikukuu ya krismasi na mwaka mpya.
Akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake alisema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi sehemu zote za ibada na viwanja vya sikukuu na halitasita kuwachukulia hatua wahalifu watakaojaribu kuchafua amani ya nchi ikiwemo kuvunja nyumba za ibada.
Aidha aliwataka wafanyabiashara kuchukua tahadhari katika mikusanyiko kwa vile baadhi ya wahalifu hutumia nafasi hiyo kutenda uhalifu ikiwemo kuiba.
Akizungunzia watu wanaokwenda kusherehekea maeneo ya fukwe za bahari aliwatahadharisha vijana kuwa makini na kwa wale wasiojua kuogelea kuwa karibu na wenye kujua kuogelea ili kuepuka madhara.
Kwa upande wa usalama barabarani, alisema jeshi hilo litahakikisha linasambaza askari wa usalama barabarani katika maeneo mbalimbali ya barabara kuu na hasa katika viwanja vitakavyosherehekewa sherehe hizo ili kuhakikisha madereva wanatii sheria bila ya shuruti.
Aliwaomba vijana waache tabia ya kuchoma moto mapira katika barabara ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya nchi na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa wahusika akiwemo sheha pindi wakigundua kama kunavijana wanaovunja amani.
Aidha aliwataka madereva kutii sheria bila ya shuruti na kuacha tabia ya kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi, kuchukua abiria kwa njia ya hatari kwani ndio chanzo cha ajali.