KAMPALA, UGANDA

MGOMBEA urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, pamoja na timu yake ya kampeni, wamekamatwa na polisi eneo la Kalangala katikati ya nchi hiyo.

Bobi Wine amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter, ambapo kukamatwa kwake kumezusha maandamano katika kisiwa cha Kalangala ambako helikopta ilitua na wafuasi wa Bobi Wine waliema wanaamini ingetumiwa kumsafirisha hadi Kampala.

Maofisa wa polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji, ambapo mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo ambaye hakutaka kutambuliwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba maofisa wa polisi walifyatua pia risasi kuwatawanya waandamanaji barabarani.

Hata hivyo polisi wamekataa kumshikilia mgombea huyo wa urais na kueleza kuwa walichokiona kwenye picha zilizopigwa kwa kutumia CCTV ni wafuasi wa mgombea huyo kuchoma matairi.

“Polisi haijamkataba Bobi Wine, tulichokiona ni kwamba wafusi wa kiongozi huyo kuchoma moto matairi ili kuzuia maofisa wa polisi wasitekeleze wajibu wao”, ilieleza taarifa ya polisi nchini humo.

Hata hivyo, huku polisi wakikataa kumkamata Bobi Wine shirika la habari la reuters, limechaisha picha zikimuonesha akiongozwa na maofisa wapatao 10 wenye silaha.

Bobi Wine ameibika kuwa mshindani mkali wa rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 14.