NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI mpya wa Chama cha Riadha Mkoa wa Pwani ( RP) umeweka wazi mikakati itakayotekelezwa katika kipindi miaka minne.

Uchaguzi wa chama hicho uliofanyika Jumapili iliyopita mkoani humo.

Akizungumza na Gazeti hili, Katibu Mkuu wa RP, Robert Kalyahe, alitaja mikakati hiyo ni kutafuta vipaji vya wanariadha vilivyo jivicha huko vijijini na skulini.

Alisema ili kufanikiwa hilo wanampango wa kuandaa mafunzo na semina zaidi kwa makocha ndani ya mkoa, ambao watabeba majukumu hayo,kufufua vipaji hasa vya akina mama ambapo ni tatizo zaidi kwa mkoa wa Pwani.

Katibu huyo alisema mkakati mwingine ni kutafuta wafadhili watakaowezesha zaidi ili kueneza riadha hadi vijijini.