KIGALI, RWANDA
RWANDA imekataa kuwakabidhi washukiwa wa jaribio la mapinduzi lililolenga kuiangusha serikali ya Burundi iliyokuwa ikiongozwa na hayati Pierre Nkurunziza lilitokea mwaka 2015.
Rwanda imekataa ombi hilo kufuatia Burundi kuwasilisha orodha ya majina ya washukiwa inaohitaji kukabidhiwa na nchi ya Rwanda kwa ajili ya kuchukuliwa hatua dhidi ya jaribio hilo la mapinduzi.
Burundi imekuwa ikiishindikizwa Rwanda kwamba moja ya sharti muhimu la kurejesha mahusiano baina ya nchi hiyo ambayo ni jirani yake ni kukabidhiwa kwa washukiwa hao.
Hata hivyo, sio Burundi wala Rwanda ambazo zimekuwa tayari kutoa orodha ya majina ya washukiwa hao, ambapo inasemekana baada ya jaribio hilo kufeli walikimbilia nchini Rwanda.
“Suala la Rwanda kuendelea kuwa na wakimbizi ni utekelezaji wa sheria za kimataifa za kuwapatia huduma wakimbizi, hata hivyo Rwanda haiwezi kuwakabidhi watu wanaojitajiwa na Burundi wakishikiwa kutekeleza mapinduzi”, alisema Manasseh Nshuti waziri wa Afrika Mashariki wa Rwnada.
Waziri huyo alisema Burundi pia ina wakimbizi wa Kinyarwanda lakini nchi hiyo haijaishindikiza ikabidhiwe, hivyo lazima nchi hizo ziheshimiane na ziheshimu sheria za kimataifa.
Miongoni mwa watu wanaotakiwa na serikali ya Burundi ni pamoja na jenerali Godefroid Niyombare ambaye ndiye anayedaiwa kuonoza mapinduzi hayo dhidi ya serikali ya Nkurunziza.