KIGALI, RWANDA

RAIS wa Rwanda Paul Kagame ametangaza kwamba askari wake wapya waliotumwa nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati ili kulinda askari wa ulinzi wa amani watafanya kazi ndani ya muda halali na wa kisheria.

Tangazo la Kagame limekuja siku moja baada ya Wizara ya ulinzi ya Rwanda kupeleka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati ikiitikia wito wa kikosi maalumu cha walinzi wa amani wa Rwanda wanaolengwa na waasi ambao waliripotiwa kuungwa mkono na rais mstaafu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize.

Rais Kagame alisema kikosi hicho kipya sio tu kitalinda askari wa Rwanda bali pia kitawasaidia wananchi.

Mgogoro wa kutumia silaha ulizuka nchini humo wiki moja kabla ya uchaguzi wake mkuu uliopangwa kufanyika Jumamosi ijayo.