NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga SC, Waziri Junior, amekanusha tuhuma za kuzizimia simu timu zinazoiwinda saini yake kwenye kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana Waziri, alikiri kuwepo kwa timu zinazomfuatilia kutaka ajiunge nazo lakini hajazima simu bali alikuwa safarini hivyo kuwa na shida ya mtandao.

Alizitaja timu hizo kuwa ni Polisi Tanzania na Ihefu FC lakini alisema yeye bado ni mchezaji wa yanga ingawa yupo katika mipango ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Misri.

“Mimisijamzimia mtu simu, nilikuwa njiani hivyo huenda mtandao ulikuwa unasumbua simu zikawa hazikamati. Zipo timu zinanihitaji lakini mwenye nina mipango ya kwenda nje,” alisema.

Waziri alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mbao FC ambayo imeshuka daraja lakini tangu aingie Jangwani hajapata nafasi sana ya kucheza.