NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya soka ya Taifa Jang’ombe imeondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Idumu ikiwa ni muendelezo wa ligi daraja la kwanza kanda Unguja.


Mchezo uliotimua vumbi majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Bungi ulikuwa wa ushindani mkubwa.
Hadi timu ya zinakwenda mapumziko Taifa ilikuwa ikiongoza mabao mawili.


Bao la kwanza liliwekwa wavuni na Abdalla Mundhir dakika ya saba na bao la pili liliongezwa na Omar Salim dakika ya 34,huku bao la tatu lilimaliziwa na Mohamed Abdalla dakika ya 67.


Mchezo mwengine uliopigwa uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 jioni timu ya Ngome iliondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwembemakubi.