NA ZUHURA JUMA
TANI 15 zimeteketezwa
katika kijiji cha Pujini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuonekana haufai kwa matumizi ya
binaadamu.
Mchele huo ulikamatwa ikiwa
unabadilishwa na kuwekwa ndani ya vipolo vya Rayyan na Asmin kwa ajili kuuzwa. Kazi hiyo ilikuwa ikifanywa katika ghala
la Kizimbani Wete.
Akizungumza baada ya kuteketezwa bidhaa hiyo na bidhaa nyengine, Mkurugenzi wa wakala wa sawa na chakula
(ZFDA) Pemba Nassir Salum Bukheti,
alisema lengo la kutekeleza bidhaa hizo ni kumlinda mwananchi.
“Leo tupo katika zoezi la kuteketeza bidhaa
ya mchele mbovu tulioukamata hivi karibuni pamoja na bidhaa nyengine ambazo
tumezipata kutokana na operesheni katika maduka
mbali mbali ndani ya mwezi huu wa Disemba,”
alisema.
Aidha alielaza bado wanaendelea na msako katika maduka na maghala ambayo yanayohifadhi mchele, ili kubaini iwapo
mchele hup uliwahi
kuingizwa kwa ajili ya kuuzwa.
Aliwataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla
kuhakikisha wanahifadhi vizuri bidhaa za chakula
kwenye
maghala na nyumba zao, ili ziwe salama kwa
matumizi ya binadamu.
Aliwataka wafanyabiashara hao kuacha udanganyifu
kwani wanakwenda kinyume na taratibu, hivyo
ikiwa kuna bidhaa imeharibika ni vyema
wakaiteketeza.
Mkuu wa idara ya udhibiti wa ubora wa chakula
kutoka
ZFDA, Saade Omar Hamad, alisema mchele huo ulibainika
haufai kwa matumizi ya binadamu na ndio sababu
wakauteketeza.
Aliwashauri wafanyabiasha wanapochukua bidhaa nyingi
waangalie na muda unaotakiwa kukaa kwa ajili ya kusambaza.
Katibu wa sheha shehia ya Pujini Kumvini, Riziki
Uledi Kombo, aliipongeza ZFDA kwa kufanya msako katika maduka na kukamata vyakula
vilivyoharibika.ya watu.
Nao wananchi walisema kuwa iwapo ZFDA
itaendeleza msako katika maduka kwa kutoa
vyakula vilivyoharibika itasaidia kuimarisha afya za wananchi.