WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani ametowa msamaha kwa watu 29 waliokuwa wakitumikia vifungo na adhabu mbalimbali, akiwemo aliyekuwa meneja wake wa kampeni, Paul Manafort, na mzazi mwenzake, Charles Kushner, ambaye ni baba wa Jared Kushner, mshauri wake mkuu na mume wa mwanawe, Ivanka.

Hatua hiyo inaifanya idadi ya watu ambao Trump aliwapa msamaha wa rais ndani ya kipindi cha siku mbili kufikia 49.

Msamaha huo unajumuisha ama kufutiwa vifungo vyao au kupunguziwa adhabu.

Pia aliwapa msamaha watu wawili ambao walitiwa hatiani kwenye uchunguzi wa Robert Mueller, wabunge wa zamani waliokuwa waungaji mkono wake na wahandisi wa zamani waliotiwa hatiani kwa mauaji ya raia nchini Iraq.