MNAMO Oktoba 30, mwaka 1961, ndege ya kuangusha mabomu iliyokuwa ikimilikiwa na Muungano wa Usovieti aina ya Tu-95 ilipaa kutoka uwanja wa kambi ya ndege za kivita ya Olenya katika rasi ya Kola kaskazini mwa Urusi.

Ndege ya Tu-95 ni kubwa sana na kwamba imeundwa kuwa na injini ambapo wahandishi wa utengenezaji ndege waliiunda mahususi kwa ajili ya kubeba mabomu.

Katika muongo mmja uliotangulia kwa wakati huo, muungano wa Usovieti ulikuwa umepiga hatua sana katika utafiti kuhusu nyuklia.

Marekani na USSR zilikuta zikiwa kwenye upande mmoja wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia, lakini baada ya vita hivyo kumalizika ndipo dunia ilipoingia kwenye kipindi cha mpito cha vita baridi.

Wasovieti baada ya kujikuta wakikabiliwa na taifa pekee lililokuwa na silaha za nyuklia, iliona njia pekee ya kushindana vyema na Marekani ni kuwa na silaha zake za aina hiyo.

Mnamo Agosti 29 mwaka 1949, Wasovieti walikwishafanya majaribio ya silaha yake ya kwanza nyuklia, ilikuwa silaha iliyopewa jina la ‘Joe-1’, majaribioa hayo yalifanyika katika nchi ambayo hivi sasa inajulikana kama Kazakhstan.

Walitumia ujuzi uliopatikana kwa siri kubwa iliyovuja kutoka kwenye mpango wa nyuklia wa Marekani, hivyo ikawa rahisi sana kwa Usovieti nayo kuwa na sialha hizo ili kujiweka tayari kukabiliana na marekani.

Miaka michache baada ya hapo nchi hiyo ilipiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya silaha za atomiki kiasi cha kufanikiwa kuwa na zaidi ya silaha 80 ya nyuklia na hadi mwaka 1958 nchi hiyo ikawa imesha fanya majaribio 36 ya nyuklia.

Katika silaha hizo zote walizokuwa nazo, hakuna bomu hata moja walilokuwa wamelifanyia majaribio, hata hivyo tayari walikwisha unda bomu lililobebwa na ndege aina ya Tu-95.

Lilikuwa bomu kubwa sana, kiasi kwamba lisingetosha eneo la kubebea mabomu kwenye nege, ambapo lililikuwa na urefu wa mita nane, kipenyo cha karibu mita 2.6 na likuwa na uzito wa tani 27.

Muonekano wake wa bomu hilo ulikuwa kama bomu lililopewa jina la ‘Little Boy’ na ‘Fat Man’, yaliyodondoshwa na Marekani katika miji ya Hiroshima na Nagasaki huko nchini Japani.

Bomu hilo lilifahamika kwa majina mengi sana kiufundi – kuna walioliita Project 27000, Product Code 202, RDS-220, na Kuzinka Mat (Mamake Kuzka), lakini sasa hufahamika zaidi kama Tsar Bomba – ‘Bomu la Tsar’.

Bomu la Tsar Bomba halikuwa bomu la kawaida la nyuklia, na lilichukuliwa kama matunda ya jaribio la wanasayansi wa USSR katika kuunda silaha ya nyuklia yenye nguvu zaidi duniani kwa wakati huo.

Wanasayansi wa usoviti walitiwa hamasa na waziri mkuu wa wakati huo nchini, Nikita Khruschchev aliyetaka nchi hiyo iwe na silaha ambayo ingeufanya ulimwengu kutikiswa na kunyenyekea.

Ilikuwa zaidi ya kifaa cha chuma ambacho hakingetoshea ndani ya sehemu ya kubebea mabomu ya ndege kubwa zaidi ya kivita, ilikuwa ni silaha ya maangamizi makubwa, silaha ya kutumiwa wakati wa mwisho kabisa.

Ndege hiyo ya Tupolev (Tu) ilikuwa imepangwa rangi nyeupe kwa makusudi ili kupunguza madhara ya mwanga ambao ungezalishwa na mlipuko wa bomu hilo.

Ndege hiyo ilifika eneo la kuangushwa bomu Novya Zemlya, eneo ambalo halikuwa na watu katika visiwa vya Bahari ya Barents juu katika kaskazini maeneo yenye barafu huko USSR.

Rubani wa ndege hiyo ya Tupolev Meja, alifikisha ndege hiyo ghuba ya Mityushikha, eneo la kufanyia majaribio silaha la muungano wa Usovieti akiwa angani umbali wa futi 34,000 sawa na kilomita 10.

Ndege nyingine ya kuangusha mabomu aina ya Tu-16 ilipaa karibu na ndege hiyo lengo lake likiwa kupiga video mlipuko wa bomu hilo na kuchunguza athari za mlipuko huo hewani ikipitia eneo la mlipuko.

Ili kuhakikisha ndege hizo mbili haziharibiwi na uwezekano wa kutodhurika ulikuwa asilimia 50, ilipangwa kwamba Tsar Bomba iangushwe kwa parachuti ya uzani wa karibu tani moja. Bomu hiyo lingeshuka hadi kiwango kilichotakikana, ambapo ni futi 13,000 na kisha kulipuka.

Wakati wa mripuko, ndege hizo za kuangusha mabomu zingekuwa karibu kilomita 50 mbali na eneo hilo, umbali huo ungetosha kuzuia ndege hizo kuathirika na mripuko.

Tsar Bomba ililipuliwa bomu hilo majira ya saa 11:32, saa za Moscow, ghafla, bomu hilo lililipuka na kusababisha moto mkubwa wa upana wa karibu maili tano.

Moto huo ulipaa angani kutoka eneo la mlipuko kutokana na nguvu za mlipuko wenyewe, mwanga wa mlipuko huo ungeonekana na watu waliokuwa umbali wa 1,000 kama maili 630.

Wingu la mlipuko lililofanana na uyoga lilipaa juu hadi kilomita 64, sehemu ya juu ikiwa imepanuka kwa karibu kilomita 100 kuanzia sehemu moja hadi nyingine, kilikuwa kitu cha kushangaza sana.

Katika eneo la Novaya Zemlya, madhara ya bomu hilo yalikuwa ya kuogofya. Katika kijiji cha Severny kilichopo umbali wa kilomita 55 kutoka eneo la mlipuko, nyumba zote ziliharibiwa kabisa.

Katika wilaya za Muungano wa Usovieti zilizokuwa mamia ya maili mbali na eneo la mlipuko, uharibifu wa kila aina ulitokea ikiwemo nyumba ziliporomoka, mapaa ya nyumba yakaanguka, vioo kwenye madirisha vikavunjika na milango ikaharibika ambapo mawasiliano ya redio yalitatizika kwa zaidi ya saa moja.

Durovtsev na ndege yake ya Tupolev walikuwa na bahati kunusurika, mlipuko wa bomu hilo ulisababisha ndege hiyo kushuka ghafla angani zaidi ya mita 1,000 kabla ya rubani kuidhibiti tena.

Mpiga picha wa Usovieti aliyeshuhudia mlipuko huo alisema baadaye: “Mawingu chini ya ndege na maeneo ya mbali yalitiwa mwanga na nuru ya ghafla yenye nguvu, mwanga huo ulienea na kuwaka hivi kwamba ungeweza kuona ndani ya mawingu”,alisema

Alisema kuwa ndege ilitokea kutoka katikati ya mawingu mawili na chini kitu kilichofanana na mpira cha rangi iliyokolea ya machungwa kilikuwa kinajitokeza, kilikuwa kitu cha kuogofya na kilifanana na sayari ya Jupiter.

Kwa sasa, inasadikiwa kwamba bomu hilo lilizalisha nishati ya megatani 57 au sawa na tani milioni 57 za TNT. Hiyo ni mara 1,500 zaidi ya mlipuko wa mabomu ya Hiroshima na Nagasaki kwa pamoja.

Aidha, ni mara kumi zaidi ya nguvu za mabomu yote ambayo yalilipuliwa wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Mlipuko kama huo haukuwa siri kwani ndege ya kijasusi ya Marekani iliyokuwa kilomita elfu kadha kutoka eneo hilo, ilikuwa na kifaa cha kupima milipuko ya nyuklia kwa mbali.

Takwimu kutoka kwa ndege hiyo zilitumiwa na wataalamu wa jopo la kufuatilia silaha za nchi za nje la Marekani kukadiria uwezo wa bomu hilo.

Muda si muda, mataifa yalianza kushutumu kitendo hicho cha USSR. Marekani na Uingereza, na hata nchi za Ulaya majirani wa muungano huo mfano Sweden.

Bahati pekee ni kwamba wingu la mlipuko huo halikufika ardhini, jambo lililosababisha kiwango cha miali iliyotokana na bomu hilo kuwa chini sana.

Aidha ni bahati kwani bomu hilo lilikuwa limefanyiwa mabadiliko kidogo kupunguza uwezo wake. Tsar Bomba ilikuwa imeundwa kuwa na uwezo mara mbili ya uliokuwa kwenye bomu hilo lilipolipuliwa.

Mmoja wa waliohusika zaidi kuunda bomu hilo alikuwa mwanafizikia Andrei Sakharov ambaye baadaye alipata umaarufu kwa kuongoza juhudi za kumaliza silaha za nyuklia ambazo alikuwa mwenyewe amechangia kuziunda na kuzistawisha.