Na Ali Othman

KAMA tunavyoona kuwa mara tu baada ya kuundwa kwa baraza la mawaziri la serikali ya awamu ya nane iliyo chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuanza kuchukua ahadi za kuwatumikia wananchi, mambo kadhaa yameanza utekelezaji wake.

Hatuna budi kumpongeza Rais wa awamu ya nane Dk.Husein Ali Mwinyi, kwa utenzi muruwa wa baraza jipya la Mawaziri wa Zanzibar, jambo ambalo kwa miaka mingi wananchi wa visiwa hivi walikuwa wakitaka utekelezaji uliotukuka.

Uteuzi huu wa mawaziri ambao lengo ni kumsaidia Rais, kiutendaji, hapana shaka umeakisi mahitaji halisi ya kiutendaji katika kuimarisha hali na uchumi  wa visiwa vya Zanzibar.

Jambo la kuvutia zaidi ni kuzipunguza wizara ambazo kwa kweli ilikuwa ni mzigo mkubwa kwa serikali, pampoja na utendaji na utekelezaji wake pia inawezekana ulikuwa ni shida kwa kiasi Fulani.

Kuzipunguza wizara ambazo zilikuwa zaidi ya 16 na sasa zipo 15, ni jambao la faraja na hasa kuirudisha tena Wizara ya Maji na Nishati huko nyuma Wizara hii ilikuwa ikijulikana kwa jina la Wizara ya Maji, Nishati na Umeme, kwa kweli ni jambo la kuitia moyo na ni wajibu na haki  wananchi wa Zanzibar  kumuunga mkono Mhe.Rais kwa juhudi zake alizozifanya kwa sasa.

Kati ya wizara hizo zipo ambazo ni mpya kama vile Wizara ya makamo wapili wa Rais Sera, Uratibu na shughuli za bara la Wawakilishi, Wizara ya Utalii na mambo ya kale na Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi.

Uwepo wa wizara hizo mpya ni kutokana na mahitaji halisi ya kiuchumi na mabadiliko ya kisera duniani. Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya dunia hivyo hapana shaka mabadiliko hayo ni muhimu sana na hasa katika utekelezaji wa sera ya CCM ya 2020/2025.

Mara baada ya kula kiapo cha utii kwa Mawaziri wote 13, huku kukiwa na wizara mbili zikisuburi wateule, hivyo hapana shaka kila waziri kufahamu wajibu wake na mipaka yake ya kazi pamoja na taasisi zilizopo chini ya wizara yake.

Rais wa Zanzibar alitoa agizo kwa mawaziri wote waliokula kiapo cha utii kutekeleza mambo kumi na tatu, ambapo si lazima leo kuyataja yote ila tunaweza kuyagusa machache tu.

Ni wajibu wa  kila Waziri kuifahamu, kuijuwa na  kuitambua wizara yake pamoja na taasisi zake zote, kuzitambua kikuwa na maana pana zaidi na hasa kiutendaji na uwajibikaji wa kila hali ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoweya.

Ni haki na wajibu wa kila Waziri kuzipitia, na kuzikaguwa nyaraka muhimu zilizopo ndnai ya afisi zao, lakini wakati wanapozitembelea taasisi pindi wakibaini mapungu na matatizo wayafanyie kazi ikiwa ni pamoja na kutafuta ufumbuzi au usuluhisho wa tatizo liliyopo badala ya kuchochea au kuwa sehemu ya migogoro hiyo kama ambavyo Dk. Kikwete alivyosema “Si vyema kurithi adui wa mtu, tafuta adui wako”.

Aidha, Rais amewataka kila Waziri au Wizara kutengeneza mpango kazi na bajeti halisi kama ambavyo imeanishwa kwenye ahadi za Rais wakati wa kampeni, ambapo kuwepo kwa mpango kazi kutasaidia kufikia malengo ya kimkakati pamoja na serikali kwa ujumla.

Mbali na hilo ni wajibu wa kila Waziri kutembelea miradi ambayo inaendeshwa na wizara yake, ikiwa ni pamoja na kuangalia ubora wa miradi hiyo, mfano mzuri hapa ni miradi ya ujenzi wa barabara ambazo zilijengwa kipindi cha kwanza na pili cha uongozi wa serikali ya awamu ya saba lakini leo hii haifai utadhani  ni barabara za miaka ya sabiini.

Lakini hata meli iliyonunuliwa na serikali kwa pesa nyingi leo ipo tu haifanyika kazi kwa kuwa  ni mbovu mbaya zaidi meli hiyo hata miaka kumi haijafaika hivyo kuna kosa la uwajibikaji na uadilifu kwa baadhi ya taasisi na watendaji wake.

Mbali ya barabara, hata taa za barabarani nazo zipo sawa na barabara zipo zinazowaka na zipo zisizo waka na tena baadhi ya taa hizo hata miaka kumi hazijafika, hii ni khatari na ipo haja kwa waziri husika kulifanyika kazi ipaswavyo, na hasi tukizingatia kwamba Zanzibar ni kituo kikubwa cha utalii Tanzania, hivyo ni wajibu wa waziri na wizara husika kufuatilia ipasavyo suala la barabara na taa zake.

Ama kuhusu suala la uwajibikaji ni jambo la muhimu sana katika jamii na hasa kupitia vyombo vya habari vya serikali na vile binafsi, ipo haja kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuwa karibu na wana habari nchini.

Lakini pia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kupitia Waziri husika kuangalia upya sheria ya vyombo vya habari, pamoja na maslahi ya waandishi wa wa habari kwa upana wake ikiwa pamoja na posho, kuongeza elimu, vitendea kazi na mambo mengine muhimu yanayohusu sekta hii na hasa katika zama hizi za sayansi ya teknoligia.

Na kwa kuwa Rais ameunda Wizara mpya ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi, ni vyema kwa  wizara husika kuwa na nguvu kazi na mipango imara ya kuimarisha wizara hii mpya.

Lengo la Rais ni kujenga na sio kumtafuta mchawi, lakini tunasema japo mwanga anaweza kutafutwa na kuondoshwa kwa maslahi mapana ya Zanzibar na watu wake.

Hakuna lisilowezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa nafasi aliyonayo.