Lucas Digne
KLABU ya Everton inaandaa kandarasi mpya kwa beki wa kushoto wa Ufaransa, Lucas Digne. Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Times).

John Stones
MLINZI wa kati wa Manchester City na England, John Stones (26), yuko mbioni kuongeza mkataba hapo Etihad baada ya kushinda karibu na meneja, Pep Guardiola, msimu huu. (Telegraph).

David Alaba
MLINZI wa Bayern Munich na Austria, David Alaba, amekataa kusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ulaya na anaweza kuzungumza na klabu nyengine kuanzia Januari. Chelsea, Real Madrid na Paris St-Germain zinavutiwa na kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Mail).

Maxi Gomez
KLABU ya Arsenal inavutiwa na kumsaini mshambuliaji wa Valencia na Uruguay, Maxi Gomez (24). (Mirror).

Marcos Rojo
KLABU ya Newcastle United na Sheffield United zinavutiwa na kumsaini beki wa Manchester United na Argentina, Marcos Rojo (30), kwa mkopo. (The Athletic).

Jan Oblak
KLABU ya Paris St-Germain inapanga ofa kwa mlinda mlango wa Atletico Madrid, Jan Oblak (27), huku nyota huyo wa kimataifa wa Slovenia ikiangalia changamoto mpya. (Mail).

Phil Jones
BEKI wa Manchester United na England, Phil Jones (28), analengwa kwa mkopo na klabu za West Bromwich Albion na Derby County. (Star).

Moses Caicedo
MANCHESTER United inataka kumsaini kiungo wa Ecuador, Moises Caicedo (19), kutoka Independiente del Valle mwezi Januari. (Manchester Evening News).

Pep Guardiola
KOCHA wa Manchester City, Pe Guardiola hatarajii kuleta mshambuliaji mpya wakati wa usajili wa Januari, licha ya Gabriel Jesus na Sergio Aguero kukosa mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton juzi. (Goal).

Rhys Williams
MLINZI wa Liverpool na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Rhys Williams (19), hataruhusiwa kuondoka kwa mkopo. Alikuwa akitafutwa na klabu nyingi za ligi daraja la kwanza, ikiwemo Middlesbrough. (Sun).

Sam Allardyce
KOCHA mpya wa West Brom, Sam Allardyce, amemkosoa kiungo wa Kiingereza, Jake Livermore na amedokeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anaweza kupoteza unahodha wa klabu baada ya kadi yake nyekundu katika kipigo cha 3-0 mbele ya Aston Villa. (Independent).

Demarai Grey
KLABU ya Leicester City inajiandaa kumruhusu winga wa Kiingereza, Demarai Grey (24), aondoke klabuni hapo Januari na Tottenham Hotspur, Everton, Southampton na Crystal Palace wanapendezwa. (90 min).

Rob Holding
KLABU ya Arsenal imefungua mazungumzo ya kandarasi na beki wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 25, Rob Holding. (Football Insider).