Ozan Kabak
MANCHESTER United na Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa ambazo tayari zimekwishaeleza nia yao ya kumchukua mlinzi wa Schalke, Ozan Kabak (20), huku klabu hiyo ya Bundesliga ikishusha bei yake na sasa ikitaka ilipwe pauni milioni 25 badala ya milioni 40 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Mail).

Jack Grealish
LIVERPOOL wamejiunga na Manchester United na Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsaini, Jack Grealish (25), huku Aston Villa wakitaka dau zito kwa ajili ya kiungo huyo wa England. (Mirror).

David Alaba
MANCHESTER United ina matumaini inaweza kuzipiku Real Madrid na Barcelona katika kusiani mkataba na mlinzi wa Austria, David Alaba (28), ambaye mkataba wake katika Bayern Munich unaisha msimu. ujao . (Mirror).

Christian Eriksen
ARSENAL wanaangalia uwezekano wa kumuhamisha kiungo wa Inter Milan na Denmark, Christian Eriksen (28), katika dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi wa Januari. (Gazzetta dello Sports).

James Tarkowski
KLABU za West Ham, Leicester City na klabu nyengine za Ligi Kuu ya England zinataka kusaini mkataba na mlinzi wa Burnley na England, James Tarkowski (29), mwezi Januari. (Eurosport).

Mo Salah
LIVERPOOL ina uhakika wa kupata ofa kutoka kwa mshambuliaji wao raia wa Misri, Mohamed Salah (28), na kumuongezea malipo yake ya pauni 200,00 kila wiki ili kuzima nia ya Real Madrid, Barcelona na Paris St-Germain ya kumchukua. (Goal).

Brandon Williams
BAYERN Leverkusen wamezungumza na Manchester United juu ya kusaini mkataba wa kudumu na beki Muingereza, Brandon Williams (20). (Sky Germany).

Adama Traore
KLABU ya Leeds United wanamtaka winga wa Hispania, Adama Traore (24), huku kukiwa hakuna uhakika wa hali yake ya usoni huko Wolves kutokana na klabu hiyo kumnyima muda wa kucheza uwanjani. (90 min).

Marcus Rashford
MGOMBEA wa wadhifa wa rais wa Barcelona, Jordi Farre, amesema, klabu hiyo inahitaji kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akamtaja mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford (23), miongoni mwa wachezaji anaowahusudu. Jordi Farre mwenye umri wa miaka 45, pia ameahidi kumsaini tena Neymar. (90 min).

Dominic Calvert-Lewin
MENEJA msaidizi wa Everton, Davide Ancelotti, amesema, mshambuliaji wa England, Dominic Calvert-Lewin (23), ana uwezo maalumu unaofanana na wa nyota wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo (35). (Talksport).

Calum Scanlon
DAU la Liverpool la kumtaka mchezaji wa timu ya vijana wadogo ya kimataifa ya England kutoka Birmingham City, Calum Scanlon limekubaliwa. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 tu anacheza upande wa kushoto wa ulinzi na pia kati kati . (Times).

Catalin Cirjan
MENEJA wa Arsenal, Mikel Arteta, amempandisha daraja la kudumu mchezaji wa timu ya taifa ya vijana wadogo ya Romania , Catalin Cirjan (18), na kumuingiza kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal . (Metro).