Mohamed Simakan
KLABU za Everton na Wolves wanatarajiwa kukabiliana na AC Milan katika kumsajili beki wa Strasbourg na Ufaransa, Mohamed Simakan (20), ambaye anapatikana kwa dau la pauni milioni 20. (Tutto Mercato Web).

Erling Braut Haaland
CHELSEA imejiunga katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland (20), lakini, Manchester City inajichukulia kuwa ndio ilio kifua mbele kumsajili mchezaji huyo. (90 min).

Dominic Calvert-Lewin
MATUMAINI ya Manchester United katika kumsajili Halaand huenda yakadhoofishwa kutokana na uhusiano wake na wakala Mino Raiola, ikimaanisha kwamba mshambuliji wa Everton, Dominic Calvert-Lewin (23), huenda akawa mbadala wa kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror).

Declan Rice
CHELSEA ina mpango wa kutoa fedha za kumsajili Haaland, na kiungo wa kati wa West Ham na England, Declan Rice kupitia kuwauza wachezaji saba, Ross Barkley (27), Marcos Alonso (29), Antonio Rudiger (27), Denmark, Andreas Christensen (24), Jorginho (29), Danny Drinkwater (30), na Victor Moses (30). (Sky Sports).

Antonio Rudiger
KLABU ya Paris St-Germain inamnyatia Antonio Rudiger, huku beki huyo akipata tatizo la kujiunga na kikosi cha kwanza katika klabu ya Stamford Bridge. (Le Parisien).

Eder Militao
LIVERPOOL ina azma ya kumsajili beki wa Real Madrid, Eder Militao (22), huku mchezaji huru wa Argentina Ezequiel Garay (34), akitarajiwa kujiunga na klabu ya Jurgen Klopp. (Todofichajes).

Vinicius Jr
KOCHA, Mikel Arteta na Arsenal, wana azma ya kumsaini mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Vinicius Jr (20), kwa mkopo mwezi Januari, lakini, wameamua dhidi ya kumsaini mchezaji mwenza na kiungo wa Hispania Isco (28), ambaye anatarajiwa kujiunga na Juventus. (Daily Star).

Shkodran Mustafi
KLABU ya Barcelona imeanza mazungumzo na beki wa Arsenal na Ujerumani, Shkodran Mustafi (28), ya uhamisho wa bila ya malipo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu. (SPOX).

Wayne Rooney
MENEJA wa Derby County, Wayne Rooney, anataka kumsaini,Phil Jones (28), akiwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili ijapokua ‘Rams’ huenda ikakabiliwa na ushindani kutoka kwa West Brom na Burnley. (Metro).

Loris Karius
KIPA, Loris Karius (27), huenda akarudi Liverpool, baada ya Union Berlin kufikiria kusitisha kandarasi yake mapema huku mchezaji hyo wa Ujerumani akichezeshwa mara moja tangu kuanza kwa msimu. (Kicker).

Ruqui Puig
KLABU ya Barcelona inajaribu kumrai kiungo wa Hispania, Ruqui Puig, kutia saini kandarasi mpy huku Manchester City na Bayern Munich zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Fichajes ).