PHIL FODEN
KIUNGO wa Manchester City Phil Foden anawindwa na Real Madrid, ambao wanaamini wangeweza kumtumia kijana huyo wa miaka 20 kwa kukosa muda wa kucheza katika timu yake ili kumleta Hispania. (Sunday Mirror)
PAUL POGBA
JUVENTUS wanafikiria uhamisho wa Januari ili kumnasa kiungo wa zamani Paul Pogba kurudi Turin, lakini watahitaji Manchester United kukubali ada ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Eurosport)
SAM JOHNSTONE
MLINDA mlango wa Uingereza wa West Brom Sam Johnstone, 27, anaweza kuwa lengo la Leeds na Brighton ikiwa Baggies watashuka kutoka Ligi Kuu. (Sun on Sunday)
MESUT OZIL
KIKOSI cha kwanza cha Arsenal kimegawanywa na uhamisho wa mchezaji mwenye umri wa miaka 32 Mesut Ozil, na kundi la wachezaji wakubwa wanaounga mkono kurudishwa kwa Mjerumani huyo. (Sunday Telegraph)
LEANDRO PAREDES
PARIS ST-GERMAIN itakuwa tayari kuipa Inter Milan kiungo wao wa miaka 26 wa Argentina Leandro Paredes kwa kubadilishana na kiungo wa Kidenmark Christian Eriksen, 28.(Le10Football – in French)
NUNO ESPIRITO SANTO
MENEJA wa Wolves Nuno Espirito Santo amemtetea winga wa kimataifa wa Hispania Adama Traore, 22, baada ya msimu kutokuwa sawa. (Sunday Mirror)
LUKA JOVIC
WOLVES inaweza kumgeukia mshambuliaji wa Real Madrid Luka Jovic, 22, au mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 25, ili kuongeza nguvu nafasi ya ushambuliaji mnamo Januari. (Express & Star)
MARCEL SABITZER
TOTTENHAM wana nia ya kumsaini kiungo wa RB Leipzig Marcel Sabitzer, 26, na klabu ya Ujerumani haitaki kuboresha makubaliano yake ya sasa ambayo yatamalizika majira ya joto ya 2022. (Bild’s Christian Falk on Twitter)
DANIEL JAMES
WEST BROM wamejiunga na Leeds, Burnley na Brighton kwa matumaini ya kumchukua winga wa miaka 19 wa Manchester United Daniel James kwa mkopo Januari. (Daily Star Sunday)
HOUSSEM AOUAR
ARSENAL wana mashaka juu ya kumsajili kiungo wa Ufaransa wa Lyon Houssem Aouar, 22, lakini wanafikiria kumchukua kiungo wa Borussia Dortmund wa Ujerumani 24 Julian Brandt.(The Athletic via Sun on Sunday)
Folarin Balogun
MSHAMBULIAJI wa Arsenal Folarin Balogun, 19, ameivutia Liverpool na timu nyingi za Bundesliga wakati mkataba wake unakaribia kumalizika. (Daily Star Sunday)
RAFAEL BENITEZ
MENEJA wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anaweza kuwa kocha wa Arsenal ikiwa klabu itaamua kumtema Mikel Arteta. (Sunday Express)
FLORIAN THAUVIN
SEVILLA na AC Milan ni miongoni mwa wale wanaotarajia kumpata mshambuliaji wa Marseille Florian Thauvin, 27, atakapokuwa mchezaji huru msimu wa joto. (A Bola – in Portuguese)