MESUT OZIL
ARSENAL wamepeana mchezaji nyota wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, kwa Juventus kwa mkopo wa miezi sita na wako tayari kupunguza marupurupu yake kuhakikisha ofa hiyo inafanikishwa. (Tuttosport via the Sun)


DAVID ALABA
MANCHESTER UNITED wamejiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, ambaye huenda akapatikana kwa uhamisho wa bure msimu ujao. Klabu hiyo ya The Old Trafford inahoji bei ya kiongo huyo raia wa Austria aliye na umri wa miaka 28 ambaye anacheza safu ya kushoto na nyuma. (The Athletic via Manchester Evening News)

TARIQ LAMPTEY
ARSENAL wana matumaini ya kuzipiku Manchester City na Bayern Munich katika mbio za kupata saini ya Tariq Lamptey, 20, kutoka Brighton, ikiwa iHector Bellerin, 25, ataamua kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Barcelona. (Daily Mirror)

GEORGINIO WIJNALDUM
KIUNGO wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ataamua kuhusu ofa ya kurefusha mkataba wake Liverpool katika muda wa siku chache zijazo. (the Guardian)

ETIENNE CAPOUE
WATFORD wameanza mazungumzo na klabu ya Villarreal ya Uhispania kuhusu uuzaji wa Etienne Capoue, inasemekana kuwa inatafuta pauni milioni 4 kumwachilia kiungo huyo wa kati raia wa Ufaransa wa aliye na umri wa miaka 32. (Daily Mail)

DAVID MOYES
MKUFUNZI wa West Ham United David Moyes ana matumaini kuwa kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21, anaweza kushawishiwa asikubali kujiunga na Chelsea kwa kupewa mkataba mpya Olympic Stadium. (Daily Mail)

PAUL POGBA
JUVENTUS wanafikiria uhamisho wa Januari ili kumnasa kiungo wa zamani Paul Pogba kurudi Turin, lakini watahitaji Manchester United kukubali dauni la pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa miaka 27.(Eurosport)

LEANDRO PAREDES
PARIS ST-GERMAIN iko tayari kuipatia Inter Milan kiungo wake wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 Leandro Paredes ili kubadilishana na kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 28 (Le10Football – in French)

HOUSSEM AOUAR

ARSENAL wana wasiwasi juu ya kumsajili kiungo wa Ufaransa na Lyon Houssem Aouar, 22, na badala yake wanafikiria kumchukua kiungo wa Borussia Dortmund na Ujerumani 24 Julian Brandt.(The Athletic via Sun on Sunday)

PHIL FODEN
KIUNGO wa kati wa Manchester City Phil Foden ndiye anayewindwa na Real Madrid, ambao wanaamini wanaweza kumtumia kijana huyo wa miaka 20 kwa kukosa muda wa kucheza kumleta Uhispania. (Sunday Mirror)

FOLARIN BALOGUN
MSHAMBULIAJI wa Arsenal Folarin Balogun, 19, anaivutia Liverpool na timu nyingi za ligi ya Bundesliga wakati mkataba wake unapokaribia kukamilika. (Daily Star Sunday)

RAFAEL BENITEZ
MENEJA wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anaweza kuwa kocha mpya wa Arsenal ikiwa klabu hiyo itaamua kumtema Mikel Arteta. (Sunday