Wilfried Zaha
KLABU ya AC Milan inasaka saini ya winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha mwezi Januari na inaamini kwamba mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 28 wa Ivory Coast anaweza kuwasaidia kupata taji la kwanza la ‘Serie A’ katika kipindi cha miaka 10. (Sun).

Gianluigi Donnarumma
AC Milan pia ina matumaini ya kuafikiana mkataba wa kumzuia kipa wa Itali mwenye umri wa miaka 21, Gianluigi Donnarumma katika klabu hiyo. (Corriere Della Sera).

Hakan Calhanoglu
KIUNGO wa Uturuki, Hakan Calhanoglu (26), anasubiri kupokea kandarasi mpya kutoka AC Milan, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na klabu zimetofautiana kuhusu mshahara. (Gazetta dello Sport).

Diego Costa
MSHAMBULIAJI wa Hispania, Diego Costa (32), ameambia Atletico Madrid anataka kandarasi yake kufutwa na kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Goal).

Sergio Ramos
MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Jose Mourinho anatumai kuungana tena na beki wa Hispania, Sergio Ramos (34) huku akichunguza mkwamo kuhusu kandarasi yake katika klabu ya Real. (Evening Standard).

Thomas Tuchel
MENEJA wa zamani wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa kumrithi, Frank Lampard katika klabu ya Chelsea. (Bild).

Isco
KIUNGO wa Hispania, Isco huenda akaondoka Real Madrid na kujiunga na Ligi Kuu ya England badala ya ile ya ‘Serie A’ huku Arsenal na Everton zikiMnyatia mchezaji huyo.(Mundo Deportivo).

Brandon Williams
KLABU ya Newcastle United huenda ikategemea usajili wa mkopo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku beki wa Manchster United na England, Brandon Williams akiwa miongoni mwa majina. (Chronicle).

Marcel Sabitzer
KOCHA, Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Marcel Sabitzer.
.(Bild).

Dele Alli
KOCHA, Mauricio Pochettino atamfanya Dele Alli kuwa mlengwa wake wa kwanza wa uhamisho ikiwa atachukua nafasi ya umeneja PSG.(Sun).

Mauricio Pochettino
MAURICIO Pochettino anataka kumtwaa, Lionel Messi kwenda PSG wakati atakapojiunga na miamba hiyo ya ‘Ligue 1’. (Le Parisien).

Chris Wondolowski
CHRIS Wondolowski amesaini nyongeza ya kandarasi ya mwaka mmoja ili kubakia na San Jose Earthquakes mnamo 2021.
Uvumi ulikuwa umeenea kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa anafikiria kustaafu, lakini ameamua kuendelea kwa angalau msimu mmoja zaidi.(Centerline Soccer).

Tukefusa Kubo
KLABU ya Getafe inaangalia kuwaleta kwa mkopo wachezaji wawili wa hali ya juu msimu huu wa baridi, Takefusa Kubo kutoka Real Madrid na Carles Alena wa Barcelona.(AS).

Wout Weghorst
KLABU ya Wolfsburg imemuahidi Wout Weghorst anaweza kujiunga na Tottenham ikiwa wataweka ofa ya pauni milioni 35.(Bild).

Jackson Irvine
KIUNGO, Jackson Irvine, anafanya mazoezi na Oldham Athletic ya Harry Kewell, lakini, hatasajiliwa na klabu hiyo ya ligi daraja la pili.