Isco
ARSENAL wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid, Isco (28), wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa. Washika bunduki hao ambao wanataka kumsaini mchezaji huyo kwa mkopo wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Sevilla. (AS).

Georginio Wijnaldum
KIUNGO wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30), ataamua wiki hii iwapo atatia saini kandarasi mpya na Liverpool huku kocha, Ronald Koeman akiwa na matumaini ya kumshawishi kiungo huyo kujiunga na Barcelona. Kandarasi ya Wijnaldum, ambaye amekuwa Anfield tangu 2016 inakamilika mwezi Juni (Sky Sports).

Lionel Messi
MANCHESTER City inabakia na matumaini kwamba itamsajili mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi (33), mwaka 2021, licha ya nahodha huyo wa Barca kusema kwamba anatumai kwamba siku moja atacheza soka nchini Marekani. (Telegraph).

Hugo Lloris
KOCHA, Mauricio Pochettino anatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wa Tottenham ikiwemo kiungo mshambuliaji, Dele Alli (24), na kipa wa Ufaransa, Hugo Lloris, iwapo kocha huyo raia wa Argentina atathibitishwa kuwa bosi Paris-St Germain. (Eurosport).

Diego Costa
WOLVES huenda ikawasilisha ombi la kumsajili Diego Costa (32), kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez (29), baada ya mshambuliaji huyo wa Hispania kukubali kusitisha kandarasi yake Atletico Madrid na kuwa mchezaji huru mwezi Januari. (Times).

Marcel Sabitzer
KLABU ya Tottenham ina azma ya kumsaini kiungo wa Austria, Marcel Sabitzer (26), mwezi Januari kulingana na klabu yake ya RB Leipzig. (Evening Standard).

Houssem Aouar
ARSENAL kwa sasa haitaimarisha azma yake ya kumnunua mchezaji wa Lyon na Ufaransa, Houssem Aouar wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa (The Athletic).

Milan Skriniar
LIVERPOOL imesitisha azma ya kumsajili beki wa kati wa Inter Milan, Milan Skriniar (25), baada ya kukasirishwa na dau la milioni 54 lililowasilishwa na klabu hiyo ya Italia. (Calciomercato).

Marcos Alonso
BEKI wa Chelsea na Hispania, Marcos Alonso (30), anatarajiwa kurudi Hipania na kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Alonso hajaichezea Chelsea tangu Septemba. (Independent).

Paulo Dybala
Mkufunzi wa zamani wa England na Juventus Fabio Capello anasema kwamba atabadilishana mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala (27),na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane (27). (Gazzetta dello Sport).

Wilfried Zaha
KLABU ya AC Milan inasaka saini ya winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha mwezi Januari na inaamini kwamba mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 28 wa Ivory Coast anaweza kuwasaidia kupata taji la kwanza la ‘Serie A’ katika kipindi cha miaka 10. (Sun).

Gianluigi Donnarumma
AC Milan pia ina matumaini ya kuafikiana mkataba wa kumzuia kipa wa Itali mwenye umri wa miaka 21, Gianluigi Donnarumma katika klabu hiyo. (Corriere Della Sera).

Hakan Calhanoglu
KIUNGO wa Uturuki, Hakan Calhanoglu (26), anasubiri kupokea kandarasi mpya kutoka AC Milan, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na klabu zimetofautiana kuhusu mshahara. (Gazetta dello Sport).