Max Aarons
MANCHESTER United wameongeza tena nia yao kwa beki wa Norwich, Max Aarons (20), lakini, wanaweza kulazimika kusubiri hadi majira ya joto kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England chini ya umri wa miaka 21. (Sun).

Georginio Wijnaldum
KLABU ya Wolves wamejiunga na mbio za kumsajili kiungo wa Liverpool raia wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30). (Gazzetta dello Sport).

Erling Braut Haaland
MGOMBEA urais wa Barcelona, Emili Rousaud amechukua hatua kumleta mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway, Erling Braut Haaland (20), kwenda Nou Camp ikiwa atachaguliwa kuwa rais mpya. (Marca).

Isco
MLENGWA wa Arsenal ambaye ni kiungo wa Real Madrid na Hispania, Isco (28), amekiri kuwa na nafasi nzuri kwa wapinzani wa London, Chelsea. (Mirror).

Jadon Sancho
KLABU ya Chelsea wamejiandaa kujiunga na Manchester United na Liverpool katika mbio za kumsajili Borussia Dortmund na winga wa England, Jadon Sancho (20). (Que Golazo).

Lionel Messi
MCHEZAJI wa Argentina, Lionel Messi (33), anaweza kubakia Barcelona hadi 2023 kabla ya kujiunga na Inter Miami ya David Beckham. Messi amenunua nyumba ya pauni milioni 7.25 huko Miami na anafikiriwa kutaka watoto wake wasome skuli nchini Marekani. (Cadena).

Timothy Fosu-Mensah
BEKI wa Manchester United na Uholanzi, Timothy Fosu-Mensah (22), amekataa mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu. (Mirror).

Sead Kolasinac
BEKI wa kushoto wa Bosnia na Herzegovina Sead Kolasinac (27), anajadili mkataba wa mkopo na klabu ya zamani ya Schalke. (Mail).

Fernando Llorente
JUVENTUS wana nia ya kumrejesha mshambuliaji mkongwe wa Hispania, Fernando Llorente klabuni hapo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kwa sasa yuko Napoli wapinzani wa ‘Serie A’. (Tuttosport).

Mahmoud Ahmed
MIAMBA ya Uturuki ya Galatasaray inataka kumsajili kiungo wa Aston Villa na Misri,Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan (26), kwa mkopo Januari. (Vatan).

Emerson Palmieri
KLABU ya Napoli wanafanyia kazi mkopo kwa beki wa pembeni wa Chelsea, Mtaliano Emerson Palmieri (26). (Corriere dello Sport).

Mat Ryan
KLABU ya Brighton imemwambia kipa wa Australia, Mat Ryan (28), yuko huru kuondoka Januari ikiwa “watapata ofa nzuri”. (Mirror).