BERLIN, UJERUMANI

HADI sasa Ujerumani imesajili vifo 962 vilivyotokana na maambukizo ya virusi vya corona ndani ya kipindi cha masaa 24.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Maradhi ya Maambukizo ya Robert Koch.

Idadi hii inavunja rikodi ya vifo vya wagonjwa wa COVID-19 kwa siku moja, iliyofikiwa wiki iliyopita ambapo watu 952 walipoteza maisha.

Kwa idadi hiyo, sasa Ujerumani ishapoteza watu 27,968 kutokana na virusi hivyo.

Watu waliosajiliwa kuambukizwa virusi hivyo kwa sasa ni 24,740.

Kwenye hotuba yake ya Krismasi iliyochapishwa jana, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, alilielezea janga la corona kama kitisho kikubwa kwa maisha ya Wajerumani.

Hata hivyo, rais huyo alisema kwamba anatiwa moyo na jinsi Wajerumani walivyosimama imara mbele ya majaribu haya, na kwamba hatimaye Ujerumani itashinda.