KHARTOUM, SUDAN

UJUMBE wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wa askari wa kulinda amani katika jimbo la Darfur huko Sudan utamaliza muda wake wa kuhudumu nchini humo mnamo Desemba 31.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa uamuzi huo ikiwa ni miaka 13 tangu kuundwa kwa ujumbe huo na kutumwa Darfur.

Baraza hilo lenye wanachama 15, limepitisha azimio hilo kwa sauti moja kusimamisha operesheni za ujumbe huo unaojulikana kama UNAMID ifikapo mwisho wa mwezi.

Aidha walikubaliana kutoa kipindi cha miezi sita, ambapo askari wote wanatakiwa kuwa wameondoka kabisa Darfur ifikapo Juni 30.