NA ABDI SULEIMAN
WAJUMBE wa baraza kuu UWT Wilaya ya Chake Chake, wametakiwa kushikiana kusaidiana katika kugombania nafasi za uongozi.
Hayo yalielezwa na aliekuwa Ofisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni, Sanaa na Michezo, Fatma Hamad Rajab wakati alipokua akifungua kikao cha baraza kuu UWT wilaya hiyo.
Alisema mshikamano, upendo na umoja ndio kitu muhimu katika maendeleo.
Alisema majungu na fitna hazimsaidi mtu yeyote katika kufikia maendeleo bora badala yake yanamrejesha nyuma.
Aidha aliwataka wajumbe wa baraza kuu UWT wilaya hiyo, kuhakikisha wanashikamana na kuwa kitu kimoja ili kutokuwapa nasafi watu wenye tabia ya ufitinishaji.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa kusini Pemba, Bimkubwa Mohamed Khamis, alisema katika mkoa huo hakuna jimbo ambalo mwanamke hawakugombea.
Aliahidi 2025 kuwa wanawake wengi watajitokeza katika kuwania nafasi za uongozi,huku akiomba kuwaungwa mkono pale watakapogombania.
Katibu wa UWT wilaya ya Chake Chake, Riziki Sadra Hassan, alisema kikao hicho kinafanyika kila baada ya miezi sita, huku kikiwa na ajenda mbili muhimu.