NA NASRA MANZI
TIMU ya Verde FC imefanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya Mapaking FC kwa bao 1-0.


Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa majira ya saa 10:15 jioni katika uwanja wa kivubo melinne Taveta.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza timu zilitoka uwanjani kwa sare ya kutokufungana.


Kurudi tena kipindi cha pili timu zilifanya mabadiliko ya hapa na pale mnamo dakika ya 48 timu ya Verde FC ilifanikiwa kupata bao lililofungwa na mchezaji Mussa Othamn Kabahe.


Baada ya kumalizika mchezo huo timu zote zilipatiwa fedha taslimu pamoja na katuni mbili za soda.
Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Mbunge wa jimbo la Dimani Mustafa Mwinyi Kondo.