NA VICTORIA GODFREY, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Mashindano ya soka ya Veterans Ubungo Super cup imesema mwisho wa kuthibitisha ushiriki na kulipa ada ya mashindano hayo Disemba 28.


Mashindano hayo yatashirikisha timu za Veterani kutoka wilaya yamepangwa kuanza kurindima Januari 9 mwakani kwenye Uwanja wa Urafiki Dar es Salaam.


Akizungumza na Gazeti hili Mtendaji Mkuu wa mashindano Franki Mchaki,alisema ada ya ushiriki ni shilingi 200,000 ambayo itatumika kwa ada ya ushiriki, gharama za uendeshaji na waamuzi.


Alisema timu 16 zitashiriki mashindano hayo, ambazo zinatakiwa kuthibitisha mapema ili kutoa fursa kwa kamati kukamilisha maandalizi.


“Viongozi wa timu shiriki wanatakiwa kujipanga na kukamilisha zoezi hili mapema, ili tuweze kukamilisha maandalizi upo mashindano yetu tuanze’’alisema


Mashindano hayo yameandaliwa na Umoja wa Maveterani wa Soka Wilaya ya Ubungo kwa kushirikiana na Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA).