DUNIA ilionekana kama imeanza kupata ahuweni kutokana na ugonjwa wa corona kwa kupatikana kwa chanjo, hatimaye hofu imezuka tena baada ya wataalamu kuthibitisha kuwepo aina mpya ya virusi vya maradhi hayo.

Aina hiyo mpya ya virusi vya corona ambayo imegunduliwa nchini Uingereza, inaelezwa kwamba vinasambaa kwa hataka sana huku nchi kadhaa kufikia sasa zikizuia usafiri wa anga nchini Uingereza.

Taarifa zinaeleza kuwa taalamu wa afya nchini Uingereza waligundua virusi vipya vya corona kutoka kwa mgonjwa mmoja mnamo mwezi Septemba mwaka huu.

Inaamikina kwamba aina hii mpya ya corona ilitokea kwa mgonjwa mmoja nchini Uingereza au imeingizwa kutoka nchi iliyo na uwezo mdogo wa kufuatilia mabadiliko ya virusi vya corona.

Aina hiyo inaweza ya virusi vya corona vinapatikana kote Uingereza, isipokuwa Ireland Kaskazini, lakini imejikita sana London, mashariki ya kusini na mashariki mwa Uingereza.

Takwimu kutoka Nextstrain, ambayo imekuwa ikifuatilia nambari za maumbile za sampuli za virusi ulimwenguni pote, zinaonyesha kuwa kesi za nchini Denmark na Australia zimetoka Uingereza.

Aina mpya ya virusi vya corona ambayo imeibuka pia nchini Afrika Kusini inaonekana kuwa na mambo kadhaa yanayolingana na hii ya Uingereza, lakini inaonekana hakuna mahusiano.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya nchini Uingereza waligundua aina mpya ya kirusi cha corona wanachoamini kinaambukiza kwa asilimia 70, ambapo tayari idara ya nchini humo imeijuulisha serikali ya Uingereza mara moja baada ya hatari yake kuthibitishwa.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alisema kutokana na aina hiyo mpya ya kirusi cha corona amelazimika kuweka masharti magumu hata katika kipindi cha sherehe za krismasi.

Kwa upande wake waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock alisema kwa sasa aina hiyo ya kirusi hakidhibitiki, lakini wanafanya kila wawezalo kukizuia kusambaa zaidi.

Hancock alisema maambukizi hayo mapya yanaonekana kuwa magumu kuyadhibti, baada ya watu zaidi ya 13,000 kubainika kuambukizwa hadi Disemba 20 mwaka huu.

Ongezeko hili limekua, licha ya Uingereza kuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutumia chanjo ya kuzuia maambukizi ya COVID-19 ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 67,000 huku wengine zaidi ya milioni wakiambukizwa.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), limesema ni kawaida ya virusi kujibadili hasa wakati kama huu ulimwengu ukigubikwa na janga la ugonjwa huo.

Maofisa wa WHO wanasema hawana ushahidi wowote unaoonyesha kwamba aina hiyo mpya ya virusi inawafanya watu kuwa wagonjwa zaidi au kuwa ni mbaya zaidi kuliko virusi vilivyokuwepo awali vya ugonjwa wa COVID-19.

Hata hivyo shirika hilo limethibitisha kwamba aina hiyo mpya inaonekana kuenea kwa kasi zaidi ikilinganishwa aina iliyokuwepo awali ya virusi vya corona.

“Kufikia sasa, ingawa tumeona mabadiliko kadhaa katika virusi vya corona, hakuna hata aina moja iliyoleta athari yoyote katika tiba zinazotumiwa kwa sasa, dawa au chanjo inayoendelea kufanyiwa uchunguzi na matumaini yetu ni kwamba hali hii itaendelea kuwa hivyo,” alisema mwanasayansi wa WHO, Soumya Swaminathan.

Habari njema zilizotangwazwa na WHO ni kwamba chanjo zilizotengenezwa na zilizoanza kutolewa za kupambana na COVID-19 zina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya aina hiyo mpya ya virusi vya corona, hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa na wanasayansi.

Uchunguzi wa awali wa aina hii mpya ya virusi umechapishwa na kubainisha mabadiliko 17 muhimu, ikiwemo kuwepo mabadiliko kwenye protini yake ya juu ya kirusi jambo ambalo ndio ufunguo ambao virusi hutumia kufungua mlango wa seli za mwili wetu.

Aina moja inayoitwa N501Y hubadilisha sehemu muhimu zaidi ya juu, inayojulikana kama kikoa kinachofungamana na mapokezi.

Hapa ndipo inafanya mawasiliano ya kwanza na uso wa seli za mwili wetu. Mabadiliko yoyote ambayo hufanya iwe rahisi kwa virusi kuingia ndani huenda ikampa makali.

Mabadiliko mengine ni kufutwa kwa H69 / V70, ambayo sehemu yake ndogo ya juu imeondolewa imeibuka mara kadhaa hapo awali, pamoja na seli maarufu iliyoambukizwa.

Kazi ya Prof. Ravi Gupta katika Chuo Kikuu cha Cambridge imedokeza mabadiliko haya huongeza maambukizi mara mbili zaidi katika majaribio ya maabara.

Uchunguzi wa kikundi hicho hicho unaonesha kufutwa hufanya kingamwili kutoka kwa damu ya waathirika kuwa na ufanisi mkubwa katika kushambulia virusi.

Prof Gupta aliniambia: “Inaongezeka kwa kasi, hiyo ndiyo sababu serikali inayo wasiwasi, tuna wasiwasi, wanasayansi wengi wana wasiwasi.”

Nchi kadhaa zimepiga marufuku usafiri wa ndege kwenda Uingereza ikiwemo Uholanzi na Ubelgiji ambapo zimepiga marufuku ndege kutoka Uingereza  kufuatia kugunduliwa kwa aina mpya ya kirusi cha corona.

Nchi nyengine duniani zimeendelea kutangaza kuzipiga marufuku ndege zao kwenda Uingereza ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa nchini humo.

Nchi zilizojiunga na orodha na mataifa kadhaa ya Ulaya ni pamoja na Kuwait, Tunisia, Urusi, Oman, Saudi Arabia pamoja na Chile.

Nchi nyingine ni Israel, El Salvador, Morocco, India, Jordan na Argentina. Mbali na Uingereza, nchi hizo zimezuia pia ndege kutoka na kwenda Afrika Kusini na Denmark, ambako kuna virusi vipya vilivyogundulika.

 Wakati huo huo, mchambuzi wa kujitegemea wa Uingereza, Dokta John Campbell ameiambia DW kwamba aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa Uingereza huenda vikaambukiza zaidi kwa asilimia 70.

Aidha, amesema sababu virusi hivyo vimekuwepo tangu mwezi Septemba, kuna uwezekano tayari vimeingia kwenye nchi kadhaa za Ulaya.