OUAKA, BAMBAR

WAASI wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamechukua udhibiti wa mji wa Bambari ambao ni wanne kwa ukubwa, kufuatia makabiliano makali ikiwa zimebakia siku tano kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.

Mashambulizi yalianza baada ya serikali kumshutumu rais wa zamani Francois Bozize kuwa anapanga njama za kufanya mapinduzi akishirikiana na makundi ya uasi kabla ya uchaguzi.

Shambulio lilianza saa nne asubuhi na kuendelea kwa takriban masaa mawili ya mapigano ya risasi kati ya waasi na wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na kikosi cha askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSCA.

Aidha kufuatia ombi la serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Urusi na Rwanda zimetuma wanajeshi na vifaa vya kijeshi kuisaidia nchi hiyo kupambana na uasi.