NEW YORK,MAREKANI

WABUNGE Marekani wameafikiana juu ya mpango wa kutoa msaada kwa mamilioni ya Wamarekani wenye thamani ya dola bilioni 900, wakati taifa hilo likiwa linakabiliwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mpango huo unajumuisha msaada wa kusambaza chanjo, pamoja na msaada wa kifedha wa ziada wa dola 300 kila wiki kwa wale waliopoteza ajira.

Uliidhinishwa jana kufuatia miezi kadhaa ya mivutano miongoni mwa wabunge wa Marekani.

Wanasiasa wa chama cha Republica na Democratic kwa miezi kadhaa wamekuwa wakilaumiana juu ya kushindwa kufikia makubaliano hayo.