ANKARA,UTURUKI

BUNGE la Uturuki limeidhinisha sheria itakayoongeza udhibiti wa serikali kwa makundi ya asasi za kiraia, ambayo inaelezwa na asasi hizo kwamba itapunguza utendaji kazi wake.

Baadhi ya vipengele vipya vilivyoanzishwa, vinaruhusu ukaguzi wa kila mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kupambana na ufadhili wa ugaidi.

Sheria hiyo pia inaipa mamlaka wizara ya mambo ya ndani kubadili wanachama wa asasi hizo, endapo watakuwa wakichunguzwa juu ya mashitaka ya ugaidi na kusitisha shughuli zake zote kwa amri ya mahakama.

Muswada huo uliopendekzwa na chama tawala cha rais Reccep Tayyip Erdogan, uliungwa mkono wabunge wa chama tawala na washirika wake.

Sheria za Uturuki za kupambana na ugaidi ni pana na zilisababisha wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati wengi wa haki za kiraia kufungwa gerezani.